MONGELLA: CCM INA WAJIBU WA KUENDELEA KUSHIKA MADARAKA KWA UTEKELEZAJI WA ILANI



NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Mongella, amesema kuwa chama kina wajibu wa kuhakikisha kinaendelea kushika madaraka kutokana na utekelezaji mkubwa wa Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025. Mongella alitoa kauli hiyo leo, Oktoba 5, 2024, kwenye mkutano maalum wa mabalozi wa mashina wa Jimbo la Mufindi Kusini, uliofanyika katika Kata ya Igowole, Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa, akiwa katika ziara ya kuimarisha chama.


Aidha, Mongella alisisitiza kuwa makatibu kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya, kata na matawi wanapaswa kushuka hadi mashina kufanya mikutano ya kuelezea shughuli mbalimbali zilizotekelezwa na serikali, kwa kuwa mabalozi ndio msingi wa chama. Alisema, “Tuna wajibu wa kuhakikisha tunaendelea kushika madaraka. Ili adhima hiyo itekelezeke, tunatakiwa kudumisha mshikamano na umoja, kwa sababu tukishikamana hakuna litakalo shindikana.”


Uchaguzi wa Serikali za Mitaa


Mongella aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili waweze kuwachagua viongozi wa CCM watakaosikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi. Katika hatua nyingine, alikabidhi majiko 2000 ya gesi kwa mabalozi wa mashina na wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo la Mufindi Kusini, kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.


Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini, David Kihenzile, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, alimshukuru Rais Samia kwa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo. Alieleza kuwa kabla ya Rais Samia kuingia madarakani, ni vijiji vitatu pekee vilivyokuwa vikipata huduma ya maji safi na salama, lakini katika kipindi cha miaka mitatu na nusu ya uongozi wake, vijiji vyote sasa vimenufaika na huduma hiyo.


Kihenzile alibainisha kuwa, “Katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Samia, ameleta fedha nyingi za kutatua changamoto za wananchi katika kata zote za jimbo.” Aidha, alimhakikishia Naibu Katibu Mkuu ushindi wa kishindo kwa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2025, kutokana na kazi kubwa aliyoifanya Rais Samia ya kuwaletea wananchi maendeleo.


Kihenzile pia alieleza kuwa Rais Samia ni kinara wa kupambana na uharibifu wa mazingira kwa kupinga matumizi ya kuni na mkaa, hivyo akawataka wananchi wote kuunga mkono jitihada hizo kwa kutumia nishati safi ya kupikia.


Awali, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Daud Yassin, aliwahakikishia washiriki kuwa mkoa wa Iringa utaongoza kwa kura nyingi za kumchagua Rais Samia kwenye uchaguzi ujao, kutokana na utekelezaji mkubwa wa Ilani ya CCM.


Azimio la Mabalozi


Kwa upande wao, mabalozi wa mashina walipitisha azimio la kumchagua kwa kishindo Mbunge wa Mufindi Kusini, David Kihenzile katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA

MAYELE AIMWAGIA SIFA LUKUKI YANGA