'Wakati Afrika imejitahidi kutokomeza Ukoloni wa Smith kule Rhodesia mimi ninayoijua kama Zimbabwe ,OAU inakabiliwa tena na changamoto kubwa na kongwe ya Ubeberu wa nchi za Magharibi.Ni bahati mbaya sana sana hili linatugawa hata ndani ya OAU.
Sisemi na sitathubutu kusema tuko wamoja kwenye hili na tuna nia thabiti ya kutokomeza ubeberu wa Magharibi dhidi ya Afrika hii ni kwasababu wako watu humo humo ndani si wenzetu katika safari hii ngumu,ila tukiamua tunaweza.
Kama kwa pamoja sisi OAU tumeweza kumkemea na kumlaani Kaburu kwa kuendesha serikali ya Kibaguzi ndivyo hivyo tuiambie Marekani na vibaraka wake wasiwe Polisi wa Dunia katika kuhukumu kila jambo na hili hatuhitaji kwenda UNO hili tutalikemea popote pale bila kuoneana aibu"
Kauli ya Dr Julius Kambarage Nyerere akiongea na BBC nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam baada ya ndege za kijeshi za Marekani kushambulia Ikulu ya Rais wa Libya Kanali Muamar Ghaddaf na kumuua mtoto wa kurithi wa Rais huyo.
Shambulio hilo linaelezwa kuwa lilikuwa ni la kulipiza kisasi baada ya ndege ya abiria ya Marekani ya Shirika la PAN AM ikiwa na abiria 198 kuangushwa katika anga la Lockbie Scotland kwa bomu lililotegwa katika redio ndogo mwaka1989.
Comments