Mshambuliaji wa klabu ya Pyramids FC Fiston Mayele, amekisifu kikosi cha timu ya soka ya Yanga Cha msimu huu, akisema ni kizuri, chenye wachezaji bora wenye njaa ya mafanikio, akikitabiria kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa. Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Mayele alisema usajili uliofanyika msimu huu, licha ya kwanza haukuwa mkubwa sana, lakini umeongeza wachezaji bora ambao wameenda kuungana na wengine wenye kiwango cha juu na kuifanya kuwa tishio si Tanzania tu bali Afrika. "Yanga imefanya usajili mzuri sana, ina wachezaji wazuri, wanacheza kwa kasi na morali kubwa, msimu uliopita walisajili vizuri na msimu huu pia wamesajiliwa wachezaji wazuri, na hili nimeshawahi kumwambia Rais wa Yanga, Injinia Hersi, nilimpongeza kwa usajili bora na yeye pia alinipongeza kwa kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu nchini Misri. "Msimu huu wameongeza wachezaji wachache ambao nawatakia kila laheri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu, kama wataendelea kupambana hivi watafanya
Comments