RAIS SAMIA APANGA FOLENI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA MKAAZI KUPIGA KURA SERIKALI ZA MITAA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amepanga foleni akishiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Sokoine, Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 11 Oktoba,2024.


Rais Samia akipata maelezo jinsi ya kujiandikisha.

Rais, Dkt. Samia akijiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Sokoine, Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 11 Oktoba,2024.




Asema ni mapumziko ya kitaifa, ili wananchi washiriki kupiga kura kikamilifu .


Asisitiza kila mwenye sifa ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  ameitangaza 27 Novemba mwaka huu, kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa ili wananchi washiriki kikamilifu kupiga kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa. 


Rais Dkt. Samia ametangaza hivyo leo tarehe 11 Oktoba 2024, alipokuwa akizungumza na Watanzania, mara baada ya kuzindua zoezi la kujiandikisha kwenye Daftari la Wakaazi kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.


Rais Dkt. Samia ambaye amejiandikisha katika Daftari la Wakaazi wa Kitongoji cha Sokoine, Chamwino Mkoani Dodoma, amesema kila Mtanzania mwenye sifa akajiandikishe kuwa mpiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na kusisitiza umuhimu wa kutofautisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, linalotumika kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, na Daftari la Wakaazi linalotumika uchaguzi wa Novemba 27, 2024. 


“Kuna ubabaifu unajitokeza wengine wanahisi wakijiandikisha kwenye daftari la Tume Huru ya Uchaguzi haina haja kujiandikisha huku tena hapana.  Tunajiandikisha kule kwa ajili ya Uchaguzi wa mwakani, lakini hapa kwenye eneo lako unachagua mwenyekiti wako wa kitongoji na kamati yake na viongozi wengine…ni daftari jingine kabisa,” amesema Dkt. Samia. 


Rais Dkt Samia amesema kuanzia leo tarehe 11 hadi 20 Oktoba, ni siku za kujiandikisha kwenye Daftari la Wakaazi, hivyo watu wajitokeze kwa wingi kuandikishwa kuwa wapiga kura, akiongeza kuwa kila aliyefikisha miaka 21, mwanamke au mwanamme, yuko mbele kwenye shughuli za maendeleo ama ana uhusiano mzuri na watu katika jamii, kujitokeza kuomba kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Serikali ya mtaa.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA

TAKUKURU YAPONGEZWA KUWA BEGA KWA BEGA NA MBIO ZA SEPESHA ZINAZOPINGA RUSHWA YA NGONO