MATATURU NA MCHANGO WAKE KUNTU MPANGO WA MAENDELEO 2025/26


 Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amepongeza Mpango wa Maendeleo 2025/2026 namna ambavyo serikali imeutekeleza. 

Akizungumza jijini Dodoma leo Novemba 5,2024 Mtaturu amesema kuwa mwaka huu  wa mwisho wa mpango wenyewe ni kujipima namna ambavyo umefanyika.

Mtaturu amesema kuwa pato la taifa limeongezeka kila mwaka hali inayoonyesha  mwenendo mzuri wa mpango wa maendeleo unaotekelezwa .

Ameongeza kuwa  SGR imeanza kuonyesha matokeo  chanya hivyo ni vizuri ikamaliziwa  vipande vilivyobaki kwani itaongeza shughuli za uchumi kwa kusaidia watu kutumia gharama ndogo kufika mbali na muda kidogo.

Aidha amesema kuwa kilimo kinagusa watu wengi na kipaumbele kimojawapo cha mpango huu ni kuhakikisha kunakuwa na uchumi shindani ambao ni shilikishi kwa wananchi hivyo mbolea, pembejeo nyingine kama mbegu na utafiti wa wapi panafaa kwa kilimo kipi na kushauri mpango uje na jibu wa kilimo cha tija ambacho ni cha umwagiliaji si kutegemea mvua.

Sambamba na hilo amegusia suala la DP World ambapo amekiri kuwa matokeo yake chanya yameonekana kwa muda mfupi kwa kupunguza meli kusubiri muda mrefu na mapato yameogezeka ambayo kwa Tanzania ni mafanikio makubwa.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MSIMAMIZI MKUU 
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE

JINSI BINTI HUYU MWANAFUNZI ANAVYOIPENDA MITI