1. Usiwahi kuvumilia dharau kutoka kwa mtu yeyote kwa sababu yoyote, ondoka hata kama ni jambo muhimu sana.
2. Usiharibu furaha yako ya sasa kwa ajili ya tukio lililopita.
3.Usimuhukumu mtu kwa kabila, itikadi ya kivyama, rangi ya ngozi, sura, jinsia, au utajiri, la sivyo utapoteza mengi maishani.
4. Usimrudie mtu aliyekusaliti, isipokuwa kama unapenda kusalitiwa tena na tena. Usaliti ni tabia, sio kosa.
5. Mheshimu mtu lakini usimuamini kupita kiasi, kuamini sana watu ni hatari kubwa
6. Daima zingatia maamuzi yako bila kujali kitakachotokea
7. Sema hapana kwa vitu usivyovipenda
8. Tenga wakati kwa ajili ya mambo yaliyo muhimu kwako na kwa familia yako.
9. Usiogope kamwe kuchukua maamuzi magumu na kufuata malengo yako.
10. Kubali makosa yako ya nyuma na uwajibikie upya
11. Ongea kwa uaminifu na fanya Kwa uaminifu. sema unachomaanisha na maanisha unachosema.
12. Jifunze kupigana na kujilinda katika hali yoyote dhidi ya mtu yeyote.
13. Kula vizuri na ili ujenge mwili wenye nguvu unaoweza kujivunia.
14. Kuwa mbunifu wa mawazo yenye nguvu kuliko kiongozi wako.
15 .siku zote epuka kubishana kwa ajili ya kugombana.
16. Ikiwa hukualikwa Katika sherehe yoyote, usiombe kwenda.
17. Usianze mahusiano yanayoanza na nitumie ela, sijala toka asubuhi, ninunulie simu, smartphone yangu imealibika
18. Acha kukimbiza Mapenzi na mara nyingi ufukuza ndoto zako.
19. Kuwa mtu hodari katika utendaji kazi , kilimo na ufugaji , biashara, ofisini, kazini, sehemu za ibada na uwe mfano kwa watoto wako.
20. Fanya ibada, usichoke kujiombea kila siku.
Comments