MBUNGE WA JIMBO APONGEZA VIJANA 32 WA MUSOMA VIJIJINI WALIOTEMBEA KWA MIGUU KUTOKA BUTIAMA HADI MWANZA*
Leo ilikuwa siku ya Kikao cha Baraza la Vijana wa CCM (UVCCM) wa Wilaya ya Musoma Vijijini. Kikao kimefanyika Kijijini Murangi, Makao Makuu ya Chama Wilaya
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, Mgeni Rasmi kwenye Kikao cha Baraza hilo, ametoa pongezi nyingi sana kwa vijana waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza, tarehe 9-13 Oct 2024.
Tarehe 14 Oct 2024, vijana hao walishiriki kwenye sherehe za uzimaji wa Mwenge wa Uhuru (Nyerere Day), Jijini Mwanza
Mbunge huyo alitoa michango ya kusaidia ushiriki wao na vijana wengine wote kwenye matembezi hayo.
*Vijana imara na shujaa:*
Vijana wote 32 wa Musoma Vijijini walifika Mwanza bila tatizo lote - pongezi nyingi kwao!
*Ushauri kwa vijana 32:*
Mbunge huyo amewashauri na kuwahimiza vijana hao waanzishe miradi ya ki-uchumi. Maeneo yenye fursa za kujiajiri na kukuza uchumi wao yameainishwa kwenye Kikao cha Baraza la UVCCM Wilaya ya Musoma Vijijini.
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa na vijana 32 wa Musoma Vijijini (UVCCM) waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza na kushiriki Nyerere Day (14 Oct) Jijini Mwanza - picha kutoka Kijijini Murangi, Musoma Vijijini
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumamosi, 21 Dec 2024
Comments