Mhe. Neema Rugangira Aonyesha Masikitiko na Shukrani Kuhusu Tukio la Ukatili Bukoba
Mbunge wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia asasi za kiraia (NGOs), Neema Lugangira amesikitishwa sana na kitendo cha kikatili cha ubakaji wa mtoto wa miaka 9 kilichotokea katika Kata ya Kitendaguro, Bukoba Mjini, Jumapili, Desemba 8, 2024.
Lugangira ametoa shukrani za dhati kwa viongozi na taasisi mbalimbali waliojitokeza kushirikiana naye kuhakikisha mtoto huyo anapata usalama.
Ametoa shukrani kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Dkt. Dorothy Gwajima, Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima, Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC), OCD, OCS, na Dawati la Jinsia Bukoba kwa msaada wa haraka na ushirikiano wa dhati waliouonesha baada ya taarifa kuhusu mipango miovu ya kumtorosha mtoto huyo kufikishwa kwake na mwananchi mnamo tarehe 17 Desemba 2024.
Kwa neema za Mungu, tarehe 18 Desemba 2024, Lugangira aliambatana na Dada Rebecca, Afisa Ustawi wa Mkoa, kuonana na familia ya mtoto huyo.
Familia imetoa shukrani kubwa kwake Lugangira kwa jitihada zake na kwa Serikali kwa msaada wa kuhakikisha mtoto huyo yuko salama chini ya uangalizi wa Idara ya Ustawi wa Jamii Bukoba.
"Tunaendelea kusimama kidete dhidi ya ukatili wa aina yoyote kwa watoto na kuhakikisha haki inatendeka. Ninatoa wito kwa jamii kushirikiana kwa karibu na vyombo husika kwa kufichua vitendo vya kikatili ili kulinda usalama wa watoto wetu," alisema Lugangira.
Comments