RAIA WA AFRIKA MASHARIKI KUFANYA KAZI KENYA BILA KIBALI

Kenya imezindua stakabadhi mpya ya kibali cha kufanya kazi nchini humo kinachotambulika kama “CLASS R” , kitakachowakubalia raia wa mataifa wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki EAC kufanya kazi bila kutozwa ada ya malipo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali ya Kenya , Jumanne 17 Desemba 2024, Waziri Kiongozi Musalia Mudavadi ambaye pia anasimamia wizara ya mambo ya kigeni, alitangaza kwamba raia wa EAC watahitajika tu kuonyesha stakabadhi za uraia wa mataifa wanayotokea.

Hatua hii inafuatia ile ya Rwanda, ambayo ni taifa la kwanza katika EAC kufutilia mbali vibali vya kazi kwa raia wa matifa ya jumuiya ya Afrika Mashariki.

Serkali ya Kenya, aidha imefanyia mabadiliko ada ya malipo ya kibali cha kazi kwa wanaofanya kazi kwa muda . Kiwango cha chini kinachohitajika kwa mfanyakazi anayetaka kufanya kazi nchini Kenya kimeshuka had idola elfu 24 za kimarekani kutoka kwa dola elfu 55 za kimarekani ambazo zilihitajika kulipwa awali.

Mabadiliko haya yanasemekana kufanya mambo kuwa rahisi kwa wafanyakazi wa kimataifa wanoishi na kufanya kazi nchini Kenya.

Bwana Mudavadi amesema kwamba mabadiliko iliyofanya Kenya ya vibali vya kazi ni njia moja ya kujiopanga kama eneo zuri la kuwavutia wafanyakazi wa kimataifa na kikanda.

“Mbali na Umoja wa Mataifa, Benki ya Dunia pia ina ofisi yake kubwa nje ya Marekani hapa Nairobi. Kwa hivyo mji huu ni muhimu kwa bara zima. Sera yetu ni kuangazia nafasi kubwa zilizopo na Ndio maana tunafanya mabadiliko haya,”alisema Waziri Musalia.

Kibali kipya cha kitengo cha R kinaazimia kufanya usawa masuala ya ada inayotozwa kwa raia wote wa mataifa wanachama wa EAC na kuwezesha uwiano wa kikazi kote.

“Uganda na Tanzania wamekuwa wafifanya hivyo, na wako mbele yetu,” alisema Bwana Mudavadi.”sasa, pia sisi hatuwatozi ada ya kibali cha kazi raia wa EAC, kwa saababu tumefanya mabadiliko ya kuboresha hali hiyo,” alisema Mudavadi



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

BREAKING NEWSSSS. WABUNGE WAPATA AJALI

π—₯π—”π—§π—œπ—•π—” 𝗬𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—™π—¨π—‘π—šπ—” 𝗠π—ͺπ—”π—žπ—” 2024 πŸ”°

MONGELLA AWATEMBELEA HOSPITALI WALIOMWAGIWA TINDIKALI

GERSON MSIGWA AREJESHWA KUWA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI

AUCHO, BACCA, BOKA WAJUMUISHWA KWENDA ALGERIA LEO