TETESI ZA SOKA ULAYA DESEMBA 22, 2024


 Napoli inamtaka Harry Maguire, mshambuliaji wa PSG Randal Kolo Muani anafuatiliwa na timu kadhaa za Ligi ya Primia, Christopher Nkunku tayari kuondoka Chelsea.

Napoli wana nia ya kumsajili beki wa kati wa Manchester United na England Harry Maguire, huku Galatasaray pia wakifuatilia hali ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 Old Trafford. (Athletic - subscription required)

Mshambulizi wa Paris St-Germain Randal Kolo Muani, 26, ana uwezekano mkubwa wa kuondoka katika klabu hiyo ya Ligi 1 mnamo mwezi Januari, huku klabu kadhaa za Ligi ya Primia zikimhitaji Mfaransa huyo (Florian Plettenberg)

Mshambulizi wa Chelsea Christopher Nkunku, 27, yuko tayari kuondoka mwezi Januari baada ya kukosa muda wa kucheza, huku Paris St-Germain, Fenerbahce na Galatasaray zote zikimhitaji mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. (TBR Football)

Tottenham wanapanga kuweka dau la pauni milioni 20 kumnunua mlinda mlango wa Burnley wa England chini ya umri wa miaka 21 James Trafford, ambaye atakuwa na umri wa miaka 22, mwezi ujao. (Mirror)

Ipswich Town na West Ham United wana nia ya kumrejesha kiungo wa kati wa Galatasaray na Morocco Hakim Ziyech, 31, kwenye Ligi ya Primia. (Fichajes)

Tottenham wanamwinda winga wa Borussia Dortmund na Ujerumani Julian Brandt, 28. (Football Transfers)

Arsenal wanasalia kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Sporting CP na Uswidi Viktor Gyokeres, 26, ingawa mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko ndiye wanayemlenga zaidi kwa sasa. (Football

Crystal Palace wanajitahidi kufikia makubaliano ya kumsajili winga wa Ujerumani Jan-Niklas Beste, 25, kutoka Benfica. (Sacha Tavolieri)

Manchester United wako tayari kushindana na Arsenal katika juhudi zao za kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 24 . (Football Insider)

Barcelona, Tottenham, Manchester United na Chelsea wote wanavutiwa na winga wa Bayern Munich na Ujerumani Leroy Sane, 28. (Sport - in Spanish)

Kipa wa zamani wa Ujerumani Manuel Neuer, 38, huenda akasaini mkataba mpya wa kusalia Bayern Munich hadi 2026. (Florian Plettenberg)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

BREAKING NEWSSSS. WABUNGE WAPATA AJALI

π—₯π—”π—§π—œπ—•π—” 𝗬𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—™π—¨π—‘π—šπ—” 𝗠π—ͺπ—”π—žπ—” 2024 πŸ”°

MONGELLA AWATEMBELEA HOSPITALI WALIOMWAGIWA TINDIKALI

GERSON MSIGWA AREJESHWA KUWA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI

AUCHO, BACCA, BOKA WAJUMUISHWA KWENDA ALGERIA LEO