TRUMP: PUTIN ANATAKA KUKUTANA NAMI HARAKA IWEZEKANAVYO


 "Rais Putin anasema anataka kukutana nami haraka iwezekanavyo," Trump alisema katika kongamano huko Arizona. "Kwa hivyo itabidi tusubiri, lakini lazima tukomeshe vita hivi. Vita hivi vinatisha, vinatisha."

Trump, ambaye atarejea Ikulu ya White House mwezi Januari, awali alisema wakati wa kampeni kwamba akichaguliwa kuwa rais anaweza kumaliza vita hivyo chini ya saa 24."

Hivi majuzi alikosoa uidhinishaji wa Biden kwa Ukraine kutumia silaha za masafa marefu zilizotolewa na Marekani kushambulia eneo la Urusi.

"Idadi ya wanajeshi waliouawa... Ni ardhi tambarare, na risasi zinapaa, risasi zenye nguvu, bunduki zenye nguvu, na kitu pekee kinachoweza kuzuia ni mwili wa binadamu," Trump alisema, akisisitiza kwamba vita vya Ukraine visingefanyika iwapo angekuwa rais wa Marekani wakati huo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

BREAKING NEWSSSS. WABUNGE WAPATA AJALI

π—₯π—”π—§π—œπ—•π—” 𝗬𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—™π—¨π—‘π—šπ—” 𝗠π—ͺπ—”π—žπ—” 2024 πŸ”°

MONGELLA AWATEMBELEA HOSPITALI WALIOMWAGIWA TINDIKALI

GERSON MSIGWA AREJESHWA KUWA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI

AUCHO, BACCA, BOKA WAJUMUISHWA KWENDA ALGERIA LEO