URUSI YAMANASA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA JENERALI IGOR KIRILLOV

Idara ya usalama ya Urusi imesema mwanamume mwenye umri wa miaka 29 kutoka Uzbekistan amezuiliwa kwa mauaji ya jenerali mkuu Igor Kirillov na msaidizi wake huko Moscow.

Luteni Jenerali Igor Kirillov, mkuu wa Kikosi cha Ulinzi cha Nyuklia, Biolojia, Kemikali, alikuwa nje ya makazi mapema Jumanne wakati kilipuzi kilichofichwa kwenye skuta kilipolipulika kwa mbali.

Idara ya usalama ya Urusi ilisema mshukiwa alisajiliwa na ujasusi wa Ukraine, kulingana na vyombo vya habari vya serikali.

Chanzo cha habari cha Ukraine kiliiambia BBC Jumanne kwamba mauaji hayo yalipangwa na idara ya usalama ya Ukraine.

Chanzo cha usalama cha Ukraine kilisema Kirillov - ambaye alikuwa mkuu wa silaha za kemikali wa Urusi - "alilengwa kimaksudi" na kilidai kuwa alitekeleza uhalifu wa kivita.

Jumatatu, siku moja kabla ya mauaji hayo, Ukraine ilimshtaki Kirillov, 54, bila kuwepo mahakamani, ikisema "alihusika na matumizi makubwa ya silaha za kemikali zilizopigwa marufuku".

Kitengo cha mahusiano ya umma cha Shirika la Ujasusi la Urusi kilisema Jumatano kwamba kijana mwenye umri wa miaka 29 "anashukiwa kufanya shambulio la kigaidi".

Taarifa ilisema wakati wa "mahojiano alieleza kwamba aliajiriwa na huduma maalum za Ukraine".

Soma zaidi:

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

BREAKING NEWSSSS. WABUNGE WAPATA AJALI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

MONGELLA AWATEMBELEA HOSPITALI WALIOMWAGIWA TINDIKALI

π—₯π—”π—§π—œπ—•π—” 𝗬𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—™π—¨π—‘π—šπ—” 𝗠π—ͺπ—”π—žπ—” 2024 πŸ”°

GERSON MSIGWA AREJESHWA KUWA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI

AUCHO, BACCA, BOKA WAJUMUISHWA KWENDA ALGERIA LEO