*Kumbukumbu:*
Naomba kuwakumbusha kwamba hivi karibuni Mbunge wa Jimbo aligawa Saruji Mifuko 150 kwa kila kijiji kinachojenga sekondari mpya. Fedha za saruji hiyo ni zile za Mfuko wa Jimbo
Kijiji cha Mmahare, Kata ya Etaro kinaenda kwa kasi nzuri na tayari kimetumia mifuko yote 150 - hongereni!
*HARAMBEE za Mbunge wa Jimbo:*
Kwenye miradi yote ya ujenzi ya Jimboni mwetu, Mbunge wa Jimbo huwa anapiga HARAMBEE kuchangia ujenzi unaofanywa kwa kutumia nguvukazi na michango ya fedha za wanavijiji.
*HARAMBEE ya Kijiji cha Mmahare:*
Wanakijiji: Saruji Mifuko 155
Mbunge wa Jimbo: Saruji Mifuko 155
Saruji Mifuko 50:
Leo, Mbunge wa Jimbo ameipatia Kamati ya Ujenzi ya Mmahare Sekondari saruji hiyo, yaani mifuko 50 kati ya 155. Wakiimaliza ipasavyo, wanaongezewa.
*Picha iliyoambatanishwa hapa inaonesha:*
Ujenzi wa msingi wa kwanza wa majengo ya Mmahare Sekondari ya Kijiji cha Mmahare, Kata ya Etaro. Ujenzi wa umsingi huo utakamilishwa leo, 10.3.2025
Hii ni sekondari ya tatu ya Kata ya Etaro!
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumatatu, 10 Machi 2025
Comments