Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa kwa siku tano zijazo, kuanzia Machi 9 hadi Machi 12, 2025, katika maeneo kadhaa ya nchi.
Angalizo hili linakuja huku kukiwa na wasiwasi wa makazi kuzingirwa na maji kutokana na mvua hizo.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na TMA, angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya:Kigoma, Katavi, Tabora, Singida, Dodoma, Simiyu, Mara, Arusha, Manyara na Kilimanjaro (Jumapili, Machi 9, 2025). Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Mtwara, Lindi, Rukwa, Mbeya, Iringa, Songwe, Njombe na Ruvuma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba (Jumatatu, Machi 10, 2025 na Jumanne,
Machi 11, 2025). Mamlaka hiyo imesema kuwa uwezekano wa kutokea kwa mvua hizo ni wa wastani, na kiwango cha athari zinazoweza kujitokeza pia ni cha wastani. Hata hivyo, TMA imetahadharisha kuwa baadhi ya makazi yanaweza kuzingirwa na maji kutokana na mvua hizo.
"Tunawaomba wananchi wote wazingatie angalizo hili na kuchukua tahadhari stahiki," alisema Mkurugenzi Mkuu wa TMA. "Ni muhimu kujiandaa kwa uwezekano wa makazi kuzingirwa na maji, na kuchukua hatua za kuzuia madhara zaidi." mwisho
Comments