NGORONGORO YATAJA MAFANIKIO LUKUKI AWAMU YA RAIS SAMIA


    Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) Dkt. Elirehema Doriye akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, jijini Dodoma Machi 10, 2025, kuelezea mafanikio ya mamalka hiyo kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


YAFUATAYO NI BAADHI YA MAFANIKIO ALIYOYATAJA KWENYE MKUTANO HUO;


YKKatika kipindi cha miaka minne tangu Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imepata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya uhifadhi, utalii, na maendeleo ya jamii. 

 

1.    UHIFADHI NA ULINZI WA RASILIMALI ZA HIFADHI

Katika kuhakikisha uhifadhi bora wa rasilimali za hifadhi, NCAA imefanikiwa kutekeleza hatua mbalimbali kama ifuatavyo:

     I.        Kudumisha Hadhi za Kimataifa

  • Mamlaka imeendelea imetunza hadhi zake za kimataifa kutoka UNESSCO kama eneo lenye urithi mchanganyiko, Biosphere Reserve na Global Geopark.
  • Eneo hili linaendelea kuwa moja ya maajabu saba ya asili barani Afrika, likiwa na miamba na sura za nchi zinazoelezea historia ya dunia na uumbaji wake.

    II.        Udhibiti wa Mimea Vamizi

  • NCAA imeendelea kudhibiti mimea vamizi katika zaidi ya hekta 5,207.5 ndani ya hifadhi. Hatua hii imeboresha uhifadhi wa wanyamapori na ikolojia yao.

     I.        Ufuatiliaji na Ulinzi wa Wanyamapori

  • Mfumo wa ufuatiliaji wa wanyamapori umeimarishwa ambapo faru 29 wamewekewa alama za masikio na vinasa mawimbi kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wao na kuimarisha ulinzi.

    II.        Udhibiti wa Ujangili

  • NCAA, kwa kushirikiana na vikosi maalum na vyombo vya usalama, imefanikiwa kudhibiti ujangili wa wanyamapori ndani na nje ya Hifadhi ya Ngorongoro na Pori la Akiba la Pololeti.
  • Matukio ya ujangili wa tembo yamepungua kutoka 25 mwaka 2020/2021 hadi tukio moja tu mwaka 2022/2023, na hakuna tukio lolote mwaka 2024.
  • Mamlaka imekamata watuhumiwa 207 wa ujangili, ambapo 175 wamefikishwa mahakamani.
  • Mitandao ya ujangili inayotumia sumu na silaha za jadi imevunjwa katika maeneo mbalimbali.
  • Mafanikio haya yanatokana na ushirikiano madhubuti na matumizi ya teknolojia za kisasa katika kulinda wanyamapori.

  III.        Kuboresha Usalama wa Wageni

·         Matukio ya uhalifu dhidi ya wageni ndani ya hifadhi yamepungua kutoka matukio 7 mwaka 2020/2021 hadi sifuri mwaka 2024 jambo linaloimarisha usalama wa watalii.

  IV.        Ujenzi wa Vituo vya Askari

  • Mamlaka imejenga vituo viwili vya askari katika Wilaya za Korogwe na Same kwa ajili ya kusaidia Serikali kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu katika maeneo ya wananchi.

   V.        Udhibiti wa Migogoro ya Mipaka

  • Ili kudhibiti migogoro ya ardhi na uvamizi wa maeneo ya hifadhi, NCAA imejenga vigingi 110 katika mipaka ya hifadhi kwa lengo la kuimarisha utambuzi wa maeneo yaliyohifadhiwa.

  VI.        Uhifadhi wa Mazingira

Mamlaka imeotesha na kugawa miche ya miti 1,150,188 katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo 
  • la kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

     I.        Ongezeko la Idadi ya Wanyamapori

  • Idadi ya faru weusi imeongezeka kwa 40% kutoka mwaka 2020 hadi 2024, kutokana na juhudi madhubuti za uhifadhi.
  • Idadi ya simba ndani ya hifadhi imefikia takriban 188.
  • Idadi ya tembo imeongezeka kutoka 800 mwaka 2020 hadi makadirio ya 1,300 mwaka 2024.

 

    II.        Kuimarika kwa Hali ya Uhifadhi katika Pori la Akiba Pololeti na Ngorongoro

·         Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeimarisha ulinzi wa rasilimali, hali iliyosaidia kudhibiti ujangili na kurejesha mfumo wa kiikolojia wa Serengeti-Masai Mara. Hatua hizi zimechochea urejeo wa uoto wa asili na malisho ya wanyamapori.

·         Matukio ya ujangili wa tembo yamepungua kutoka 25 mwaka 2020 hadi sifuri mwaka 2024 katika Ngorongoro na Pololeti. Kwa kushirikiana na vikosi vya usalama, NCAA imefanikiwa kukamata watuhumiwa 207 wa ujangili, huku mitandao ya ujangili kwa sumu na silaha za jadi ikidhibitiwa.

·         Aidha, ili kukabiliana na changamoto za uhifadhi katika maeneo jirani, NCAA imewezesha upimaji na uandaaji wa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi kwa vijiji 36, ndani ya eneo la km² 2,500.

·         Hatua hizi zimeleta mafanikio makubwa katika uhifadhi endelevu wa Ngorongoro na Pori la Akiba Pololeti.

 

  III.        Upandikizaji wa Faru Weupe

  • Mwezi Machi 2025, Mamlaka imepandikiza faru weupe ndani ya Kreta ya Ngorongoro ikiwa ni lengo la kusaidia kuhifadhi wanyama hawa adimu ambao wako kwenye hatari ya kutoweka duniani pamoja na faru weusi ambao Kreta ya Ngorongoro inasifika kwa kuwa mahali salama kwa faru hawa.
    • Mamlaka, baada ya kufanya tafiti kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), ilijiridhisha kuwa eneo la Kreta ni salama na bora kwa ustawi wa wanyama hawa.
    • Kwasasa, faru hawa wanaendelea vizuri bila changamoto yoyote.1.    ONGEZEKO LA IDADI YA WATALII NA MAPATO YA SERIKALI

      Hifadhi ya Ngorongoro ni moja ya maeneo yanayotembelewa na watalii wengi nchini Tanzania kutokana na vivutio vyake vya kipekee, vikiwemo mandhari ya kuvutia, wanyamapori wengi, na historia ya kipekee ya kiutamaduni na kiakiolojia. Hali hii imepelekea hifadhi hii kuwa moja ya vivutio vinavyochangia asimilia kubwa ya watalii wanaokuja nchini.

       

      Takwimu zinaonesha kuwa kati ya Julai 2021 hadi Februari 2025, jumla ya watalii 2,916,540 wametembelea vivutio vya utalii ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. Katika kipindi hicho, mapato ya shilingi 693,959,894,001 yamekusanywa na kuingia kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Mchanganuo wa mapato hayo kwa kila mwaka wa fedha ni kama ifuatavyo:

      • Mwaka wa fedha 2021/22
        • Idadi ya watalii: 425,386 (Watalii wa nje: 228,810, Watalii wa ndani: 196,576)
        • Mapato yaliyokusanywa: TZS 91,131,434,280.54
      • Mwaka wa fedha 2022/23
        • Idadi ya watalii: 752,232 (Watalii wa nje: 458,351, Watalii wa ndani: 293,881)
        • Mapato yaliyokusanywa: TZS 171,257,737,653.10
      • Mwaka wa fedha 2023/24
        • Idadi ya watalii: 908,627 (Watalii wa nje: 553,875, Watalii wa ndani: 354,752)
        • Mapato yaliyokusanywa: TZS 219,547,542,813
      • Mwaka wa fedha 2024/25 (Julai – Februari 2025)
          • Idadi ya watalii: 830,295 (Watalii wa nje: 509,610, Watalii wa ndani: 320,685)
          • Mapato yaliyokusanywa: TZS 212,023,179,255.68

         

        Katika mwaka 2024/25 mwenendo unaonyesha Mamlaka itapata watalii zaidi ya Milioni moja na mapato zaidi ya lengo ambalo iliweka ambalo ni kukusanya Bilioni 230 ambapo hadi sasa katika mapato haya imeshakusanya asilimia 92.

         

        Takwimu hizi zinaonesha kuwa juhudi za Mheshimiwa Rais kupitia filamu za Royal Tour na Amazing Tanzania zimechangia kutangaza nchi yetu na kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea vivutio vyetu vya utalii. Vilevile, mikakati mbalimbali ya shirika pamoja na ushirikiano kati ya sekta binafsi na mamlaka za utalii umechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko hili.

         


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

RAIS TRUMP ARARUANA NA RAIS WA UKRAINE

MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA

SERIKALI YALIKUBALI OMBI LA DIAMOND

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO

ARAJIGA AULA KOMBE LA DUNIA