TRA YAKUSANYA ZAIDI YA SH. TRIL. 21 AWAMU YA RAIS SAMIA

KATIKA kipindi cha miaka minne ya  uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita wa Rais Samia Suluhu Hassan, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imejimwambafai kwamba imefanikiwa kukusanya kiasi cha sh. trilioni. 21.20 sawa na ufanisi wa asilimia 104, ya lengo la kukusanya sh. trilioni 20.42.


Mafanikio hayo yameelezwa na Kamishna wa TRA, Yusufu Mwenda katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, jijini Dodoma Machi 12, 2025, kuhusu mafanikio ya mamlaka hiyo kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


Amesema kuwa ulipaji kodi kwa hiari umeongezeka miongoni mwa Walipakodi. Ongezeko la makusanyo mwaka hadi mwaka unaakisi mafanikio ya uongozi wake, Kwa kipindi cha miezi nane kuanzia mwezi Julai 2024 mpaka Februari 2025,
TRA  ambao ni ukuaji wa asilimia 17 ukilinganisha na kiasi cha sh. trilioni 18.06 kilichokusanywa kipindi kama hicho mwaka wa fedha uliopita, 2023/24.


 "Makusanyo haya ni sawa na ongezeko la sh. trilioni 9.28 ambalo ni ukuaji wa asilimia 78 ukilinganisha na kiasi cha sh. trilioni 11.92 kilichokusanywa kipindi cha mwezi Julai 2020 mpaka Februari 2021, kabla ya Mhe Rais kuingia madarakani."Amesema Kamishna Mkuu Mwenda.

 Mafanikio haya yametokana na utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoyatoa wakati akimuapisha Kamishna Mkuu, Bw. Mwenda mnamo Mwezi Julai Mwaka 2024.













 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

RAIS TRUMP ARARUANA NA RAIS WA UKRAINE

MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA

SERIKALI YALIKUBALI OMBI LA DIAMOND

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO

ARAJIGA AULA KOMBE LA DUNIA