Klabu ya Young Africans imetoa msimamo mkali kutokana na lile kinachozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii. Kwa muujibu wa barua iliyotumwa kwa umma iliyoandikwa na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Inasema kuwa mchezo wa derby ya Kariokoo upo pale pale.
"Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutaarifu Umma kuwa, mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC, uliopangwa kuchezwa leo tarehe 8/3/2025, dhidi ya Simba SC, saa 1:15 usiku upo palepale na hakuna mabadiliko yoyote.
"Young Africans SC kama wenyeji wa mchezo, tunaamini taratibu zote za mchezo kama inavyoelekezwa kwenye kanuni za Ligi Kuu ya NBC, ziko sawa na maandalizi yote yako tayari.
Uongozi wa Young Africans SC utapeleka timu uwanja wa Benjamin Mkapa kama inavyoelekezwa kwenye kanuni, na hatutakuwa tayari kucheza mchezo huu siku nyingine tofauti na leo.
Tunawaalika uwanjani Wanachama, Mashabiki, Wapenzi wa Klabu yetu na Wadau wengine waliosafiri kutoka mikoani, nchi za jirani na sehemu mbalimbali duniani kote kuja kushuhudia mchezo huu mkubwa Barani Afrika. Imetolewa na Mtendaji Mkuu
Andre Mtine.


Comments