KAMWE USIWAAMINI WATU WAFUATAO!!


1. Wanaosaliti WENGINE KWASABABU wewe unaweza kuwa ndiye unayefuata kusalitiwa.

2. Wanaodanganya WENGINE KWASABABU wewe unaweza kuwa ndiye unayefuata kudanganywa.

3. Wanaowaumiza wengine kwa namna yeyote ile. Haupaswi kucheka nao kabisa kwasababu wewe ndiye unaweza kufuata kuumizwa na wao. Jitenge au usijenge mazoea au ukaribu nao!

4. Wanaokufanyia mabaya(kukudanganya,kukufokea, kukuibia mke au mume) halafu wanakwambia kuwa WANAKUTANIA. 

5. Wanaokutafuta au kuwa karibu na wewe wakati wa shida tu!( Ukiwa mgonjwa au umefiwa na mtu wako wa karibu, ukiwa umepata majanga ya ajali, umeibiwa au umepoteza kazi au biashara). Watu hawa wanajionyesha kwako kwenye matatizo yako na hawaonyeshi jitihada zozote za kukusaidia(kuchangia mchango wa pesa,ushauri au kukufariji) na wanakuwepo tu ili waonekane. Saikolojia inasema! Mara nyingi watu wa aina hii ni maadui zako ambao wanapendezwa na MATATIZO yako lakini wamejificha kwenye kivuli cha urafiki na KUKUFAHAMU. Waepuke

Mwalimu Hakika
0767552547
Kigoma, TZ.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MAKUNDI YA VILABU VINAVYOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2025.

JINSI YA KUMTAWALA MWANAMKE HASA MKE (USIOE MKE WA MTU)

MUONEKANO WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA MSALATO

DIARRA KIPA BORA TANZANIA

CHINYELE ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE DODOMA MJINI