Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paulo Chacha amewatoa hofu walaji wa asali inayozalishwa mkoani humo kwamba iko safi, tofauti na inavyoenezwa kwamba ina kemikali ya Tumbaku.
Amesema kuwa Ili kuepukana na athari hiyo, Mkoa umetenga kwa umbali maeneo ya kilimo Cha Tumbaku na misitu ya uzalishaji wa asali.
RC. Chacha amebainisha hilo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma Julai 11, 2025, kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Mkoa huo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
"Kawaida ya nyuki hawana uwezo wa kutafuta chakula umbali wa zaidi ya Km 5, ndiyo maana misitu ya kufugia nyuki imetenganishwa kwa umbali mrefu na mashamba ya tumbaku,"amesema RC Chacha.
Ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kwenda mkoani humo kuwekeza, kwani ipo misitu mingi inayofaa kwa ufugaji wa nyuki na kwamba asali ya Tabora ina ubora unaostahili.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
0754264203
Comments