TWIGA STARS YATOKA SARE NA AFRIKA KUSINI

TIMU ya Tanzania  imetoka sare ya kufungana bao 1–1 na mabingwa watetezi, Afrika Kusini katika mchezo wa Kundi C Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2024 usiku huu Uwanja Honneur mjini Oujda nchini Morocco.
Tanzania ‘Twiga Stars’ ilianza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji Opah Clement Tukumbuke wa  Juárez ya Mexico dakika ya 24, kabla ya beki wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Bambanani Nolufefe Mbane kuisawazishia Banyana Banyana dakika ya 70.
Ikumbukwe mchezo wa kwanza wa Kundi hilo Mali pia ilitoa sare kama hiyo ya 1-1 na Ghana Uwanja wa Manispaa ya Berkane.
Kwa matokeo hayo, Afrika Kusini na Mali zinafikisha pointi nne kila moja kufutia kuanza kwa kushinda mechi zao za kwanza dhidi ya Tanzania na Ghana ambazo kila moja ina pointi moja sasa.
Mechi za mwisho za Kundi C; Tanzania itamenyana na Ghana Uwanja wa Manispaa ya Berkane na Mali dhidi ya Afrika Kusini Uwanja wa Honneur zote zikianza muda mmoja, Saa 3:00 usiku.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MAKUNDI YA VILABU VINAVYOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2025.

JINSI YA KUMTAWALA MWANAMKE HASA MKE (USIOE MKE WA MTU)

MUONEKANO WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA MSALATO

DIARRA KIPA BORA TANZANIA

CHINYELE ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE DODOMA MJINI