WAZIRI KIKWETE AONGOZA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI LONGIDO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, ameongoza uzinduzi wa Mradi wa Maji katika Wilaya ya Longido,  Julai 10 wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2025.

Aidha, Mhe. Kikwete amempongeza Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg. Ismail Ali Ussi, pamoja na timu nzima ya wakimbiza mwenge kwa kazi kubwa na ya kizalendo wanayoifanya.

Amesema kupitia mbio hizo, vijana hao wameendelea kuhamasisha maendeleo, kueneza ujumbe wa matumaini kwa jamii, na kufika katika maeneo ambayo matumaini yalikuwa yameanza kufifia, hivyo kuamsha ari na mshikamano wa kitaifa.

Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ali Ismail Ussi, amesema mwenge huo umekuwa chachu ya maendeleo nchini kwa kutembelea na kuzindua miradi mbalimbali, ikiwemo mradi huu wa maji uliokamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Mradi huo unatarajiwa kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa eneo hilo na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.










 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MAKUNDI YA VILABU VINAVYOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2025.

JINSI YA KUMTAWALA MWANAMKE HASA MKE (USIOE MKE WA MTU)

MUONEKANO WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA MSALATO

DIARRA KIPA BORA TANZANIA

CHINYELE ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE DODOMA MJINI