Matukio katika Picha wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipotembelea Banda la Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari-JAB lililopo katika Kijiji cha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Julai 04 2025 jijini Dar es Salaam. Akiwa katika Banda hilo Mhe. Kikwete amekutana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi Wakili Patrick Kipangula aliyemuelezea historia fupi ya kuanzishwa Bodi hiyo, majukumu yake na maendeleo ya zoezi la usajili wa Waandishi wa Habari na ugawaji wa vitambulisho vya uandishi wa habari kwa waliokidhi vigezo vya kisheria.
DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI
Mwanaume nisikilize! Umasikini unauma zaidi ukiwa mwanaume. Familia inakutazama tofauti sana hata kama haikuambii ila we fahamu tu kuwa kuna vile wanawaza na kukutazama. Ukiwa huna pesa kuna namna fulani watu wanakunyima heshima au wanakukadiria heshima. Ukiwa huna pesa hakuna anayejali unachosema haijalishi unasema point au jambo la maana kiasi gani. Na ukiendelea kutoa msisitizo ili point yako isikilizwe utaambiwa unapiga kelele au unaleta vurugu kwenye kikao. Tunaishi katika Dunia ambayo haina huruma kwa mwanaume asiye na pesa. Dunia ni sehemu katili kwa mwanaume masikini si Kanisani si hospitalini kama huna pesa wewe si lolote si chochote hata aina ya maombi utakayopewa na heshima utakayopewa ni tofauti sana. Hata Kanisani wewe hata uwe na wanawake 6 na vimada 6 lakini una hela heshima yako italindwa, lakini kama huna pesa utatengwa. Hata Kanisa haliwapi kipaumbele wala heshima watu wasio na pesa. Mwanaume amka kila siku ufanye kazi kwa bidii na kwa akili na maarifa — du...
Comments