UMD WACHUKUA FOMU ZA URAIS WAAHIDI KUJA NA SERA YA MAJIMBO


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya kupitia tiketi ya Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD), Mwajuma Noty Mirambo. Mgombea huyo aliambatana na Mgombea Mwenza,  Mashavu Alawi Haji (kushoto).

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu, Mgombea pendekezwa wa Urais wa chama hicho, Mirambo amesema kuwa  UMD itahakikisha inainua uchumi wa Nchi na wa mmoja mmoja. Wanaamini katika sera za majimbo ambapo kila mtu atafurahia uchumi katika eneo lake na hakuna mtu atajutia kuzaliwa Tanzania.

Vyama vingine vilivyochukua fomu leo ni; na Mashavu Alawi Haji pamoja na Chama cha Tanzania Labour Party (TLP),Chama cha Tanzania Democratic Alliance ( ADA-TADEA), ambacho mgombea urais ni Georges Gabriel Bussungu ambaye aliambatana na Mgombea Mwenza,  Ali Makame Issa.

Wagombea wengine waliochukua fomu jana Agosti 10 ni;  Chama cha MAKINI ambacho wagombea wake ni Coster Jimmy Kibonde. na Mgombea Mwenza, Aziza Haji Suleiman,  National League for Democracy (NLD),  Doyo Hassan Doyo na Mgombea Mwenza,  Chausiku Khatib Mohamed na United Peoples Democratic Party (UPDP),  Twalib Ibrahim Kadege (Urais),  Mgombea Mwenza, Abdalla Mohd Khamisi.

Vyama vilivyofungua pazia ya uchukuaji fomu Agosti 9, 2025 ni; Chama Cha Mapinduzi (CCM) mgombea wake wa Urais ni Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza, Dkt. John Nchimbi, Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) walikuwa ni Hassan Kisabya Almas (Rais). na Mgombea Mwenza,  Hamisi Ally Hassan pamoja na Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP), Kunje Ngombale Mwiru (urais). Mgombea huyo wa AAFP aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe.  Shum Juma Abdalla.


 Tume inataraji kufanya uteuzi wa wagombea Agosti 27 mwaka huu na kampeni zitaanza Agosti 28 hadi Oktoba 28, 2025. Uchaguzi Mkuu wa  Rais, wabunge na madiwani utafanyika Oktoba 29.
Baadhi ya wafuasi wa UMD wakishuhudia uchukuaji wa fomu hizo.
Waandishi wa habari wakiwajibika kuripoti tukio hilo.
Wagombea wakionesha mfuko wenye fomu.

Mgombea Urais wa chama hicho akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu.




Wafuasi wakishangilia huku wakiusindikiza msafara wa magari ya wagombea.

 



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE....