SAU WACHUKUA FOMU ZA URAIS INEC, WAAHIDI KUPUNGUZA GHARAMA ZA UMEME, NISHATI

Wapendekezwa wa kugombea urais na umakamu wa Rai kupitia Chama Cha Sauti ya Umma (SAU) wakiwa na wafuasi wao wakitoka baada ya kuchukua fomu za kuomba uteuzi wa kugombea nafasi hizo katika Makao Makuu ya Tume Huru ya Taifa (INEC), Njedengwa jijini Dodoma Agosti 13, 2025.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Paul Kyara na aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Satia Mussa  Bebwa (kushoto) katika tukio lililofanyika  Agosti 13, 2025 Njedengwa jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima.


Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu, Mgombea pendekezwa wa Urais wa chama hicho, Kyara amesema kuwa atawataka watanzania kuwa na hofu ya Mungu pia wawe na uzalendo, haki na uadilifu ili kufikia malengo.

Amesema serikali yake itasisitiza matumizi ya Nishati mbadala na kupunguza gharama ya umeme na  mafuta ili  bei yake iwe nafuu hadi vijijini.

 Chama kingine kilicho kilichochukua leo asubuhi  fomu za Urais na umakamu wa Rais ni; Chama cha Democratic Party (DP), Abdul Juma Mluya (URAIS) na aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Masoud Abrahman Khatib (kushoto). Chama Cha  The Civic United Front (CUF) Chama Cha Wananchi, kitahitimisha  kuchukua fomu majira. 

Vyama vingine vilivyochukua fomu leo ni; Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD) ambacho mgombea wake Urais ni Mwajuma Noty Mirambo aliyeambatana na Mgombea Mwenza,  Mashavu Alawi Haji pamoja na Chama cha Tanzania Democratic Alliance ( ADA-TADEA), ambacho mgombea urais ni Georges Gabriel Bussungu ambaye aliambatana na Mgombea Mwenza,  Ali Makame Issa.

Wagombea wengine waliochukua fomu juzi Agosti 10 ni;  Chama cha MAKINI ambacho wagombea wake ni Coster Jimmy Kibonde. na Mgombea Mwenza, Aziza Haji Suleiman,  National League for Democracy (NLD),  Doyo Hassan Doyo na Mgombea Mwenza,  Chausiku Khatib Mohamed na United Peoples Democratic Party (UPDP),  Twalib Ibrahim Kadege (Urais),  Mgombea Mwenza, Abdalla Mohd Khamisi.

Vyama vilivyofungua pazia ya uchukuaji fomu Agosti 9, 2025 ni; Chama Cha Mapinduzi (CCM) mgombea wake wa Urais ni Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza, Dkt. John Nchimbi, Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) walikuwa ni Hassan Kisabya Almas (Rais). na Mgombea Mwenza,  Hamisi Ally Hassan pamoja na Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP),Kunje Ngombale Mwiru (urais). Mgombea huyo wa AAFP aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe.  Shum Juma Abdalla.


Tume inataraji kufanya uteuzi wa wagombea Agosti 27 mwaka huu na kampeni zitaanza Agosti 28 hadi Oktoba 28, 2025. Uchaguzi Mkuu wa  Rais, wabunge na madiwani utafanyika Oktoba 29.


Wagombea wakiwa na mfuko huo baada ya kukabidhiwa.
Kailima akiwaelekeza wagombea jinsi ya kujaza kwenye kitabu cha kumbukumbu.
 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE....

RAIS SAMIA AMUONDOLEA POLEPOLE HADHI YA UBALOZI