Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC), Wilson Elias Mulumbe (katikati) aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Shoka Khamis Juma (kushoto) katika tukio lililofanyika Agosti 14, 2025 Njedengwa jijini Dodoma.
Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu, Mgombea pendekezwa wa Urais wa chama hicho, Mulumbe amesema kuwa chama chake kikishinda atahakikisha anafuta madeni yote wanayodaiwa wanafunzi na Bodi ya Mikopo, itakuwa elimu bure, afya bure na wateja wataunganishiwa umeme bure.
Vyama vingine vilivyochukua fumu jana Agosti 13, 2025 ni; Chama cha Democratic Party (DP), Abdul Juma Mluya (Urais) aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Masoud Abrahman Khatib na Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Paul Kyara (Urais) aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Satia Mussa Bebwa.
Vilivyochukua fomu Agosti 12, 2025 ni; Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD) ambacho mgombea wake urais ni Mwajuma Noty Mirambo aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Mashavu Alawi Haji pamoja na Chama cha Tanzania Democratic Alliance ( ADA-TADEA), ambacho mgombea urais ni Georges Gabriel Bussungu aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Ali Makame Issa.
Wagombea wengine waliochukua fomu Agosti 10, 2025 ni; Chama cha MAKINI ambacho wagombea wake ni Coaster Jimmy Kibonde. na Mgombea Mwenza, Aziza Haji Suleiman, National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo (Urais) na Mgombea Mwenza, Chausiku Khatib Mohamed pamoja na United Peoples Democratic Party (UPDP), Twalib Ibrahim Kadege (Urais), Mgombea Mwenza, Abdalla Mohd Khamisi.
Vyama vilivyofungua pazia ya uchukuaji fomu Agosti 9, 2025 ni; Chama Cha Mapinduzi (CCM) mgombea wake wa Urais ni Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza, Dkt. John Nchimbi, Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) walikuwa ni Hassan Kisabya Almas (Rais). na Mgombea Mwenza, Hamisi Ally Hassan pamoja na Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP),Kunje Ngombale Mwiru (urais). Mgombea huyo wa AAFP aliambatana na Mgombea Mwenza, Shum Juma Abdalla.Hadi leo hii vyama vilivyochukua fomu ni 12.
Mulumbe akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu.
Wafuasi wa chama hicho wakishangilia baada ya wagombea wao kuchukua fomu.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments