Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha The Civic United Front (CUF), Chama Cha Wananchi, Gombo Samandito Gombo na aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Husna Mohammed Abdalla (kushoto) katika tukio lililofanyika Agosti 13, 2025 Njedengwa jijini Dodoma.
Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu, Mgombea pendekezwa wa Urais wa chama hicho, amesema kuwa chama hicho kikipata ushindi kitahakikisha wananchi wanapata stahiki zao bila kubagua kati ya wenye nacho na wasio nacho. Pia wataboresha sekta ya afya, elimu na huduma zinginezo muhumi katika jamii.
Vyama vingine vilivyochukua fumu leo ni; Chama cha Democratic Party (DP), Abdul Juma Mluya (Urais) aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Masoud Abrahman Khatib na Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Paul Kyara (Urais) aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Satia Mussa Bebwa.
Vilivyochukua fomu jana Agosti 12, 2025 ni; Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD) ambacho mgombea wake urais ni Mwajuma Noty Mirambo aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Mashavu Alawi Haji pamoja na Chama cha Tanzania Democratic Alliance ( ADA-TADEA), ambacho mgombea urais ni Georges Gabriel Bussungu aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Ali Makame Issa.
Wagombea wengine waliochukua fomu Agosti 10, 2025 ni; Chama cha MAKINI ambacho wagombea wake ni Coaster Jimmy Kibonde. na Mgombea Mwenza, Aziza Haji Suleiman, National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo (Urais) na Mgombea Mwenza, Chausiku Khatib Mohamed pamoja na United Peoples Democratic Party (UPDP), Twalib Ibrahim Kadege (Urais), Mgombea Mwenza, Abdalla Mohd Khamisi.
Vyama vilivyofungua pazia ya uchukuaji fomu Agosti 9, 2025 ni; Chama Cha Mapinduzi (CCM) mgombea wake wa Urais ni Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza, Dkt. John Nchimbi, Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) walikuwa ni Hassan Kisabya Almas (Rais). na Mgombea Mwenza, Hamisi Ally Hassan pamoja na Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP),Kunje Ngombale Mwiru (urais). Mgombea huyo wa AAFP aliambatana na Mgombea Mwenza, Shum Juma Abdalla.Hadi leo hii vyama vilivyochukua fomu ni 12.
Tume inataraji kufanya uteuzi wa wagombea Agosti 27 mwaka huu na kampeni zitaanza Agosti 28 hadi Oktoba 28, 2025. Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utafanyika Oktoba 29.
Mmmoja wa wazee wafuasi wa chama hicho akionesha furaha yake baada fomu kuchukuliwa.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments