CCK WACHUKUA FOMU ZA URAIS, WAAHIDI KUWAJENGEA NYUMBA WASTAAFU

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Kijamii (CCK), David Daud Mwaijojele na aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Masoud Ali Abdalla (kushoto) katika tukio lililofanyika  Agosti 12, 2025 Njedengwa jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima.


Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu, Mgombea pendekezwa wa Urais wa chama hicho,Mwaijojele  ameipongeza Tume kwa ushirikiano na utaratibu wao mzuri kabla na wakati wa kuchukua fomu.

Ametaja vipaumbele vyao kuwa ni; Kilimo cha kisasa, Afya, Ajira  na hasa kwa wastaafu ambao watakaowawekea uratatibu mzuri wa kudunduliza michango yao wakiwa kazini na kuwajengea nyumba watakaoishi baada ya kustafu. Pia utaraibu huo wataufanya kwa waandishi wa habari.

Vyama vingine vinavyotarajiwa kuchukua fomu za Urais na umakamu wa Rais ni; Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) na Alliance for Democratic Change (ADC).

Vyama vingine vilivyochukua fomu leo ni; Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD) ambacho mgombea wake Urais ni Mwajuma Noty Mirambo aliyeambatana na Mgombea Mwenza,  Mashavu Alawi Haji pamoja na Chama cha Tanzania Democratic Alliance ( ADA-TADEA), ambacho mgombea urais ni Georges Gabriel Bussungu ambaye aliambatana na Mgombea Mwenza,  Ali Makame Issa.

Wagombea wengine waliochukua fomu juzi Agosti 10 ni;  Chama cha MAKINI ambacho wagombea wake ni Coster Jimmy Kibonde. na Mgombea Mwenza, Aziza Haji Suleiman,  National League for Democracy (NLD),  Doyo Hassan Doyo na Mgombea Mwenza,  Chausiku Khatib Mohamed na United Peoples Democratic Party (UPDP),  Twalib Ibrahim Kadege (Urais),  Mgombea Mwenza, Abdalla Mohd Khamisi.

Vyama vilivyofungua pazia ya uchukuaji fomu Agosti 9, 2025 ni; Chama Cha Mapinduzi (CCM) mgombea wake wa Urais ni Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza, Dkt. John Nchimbi, Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) walikuwa ni Hassan Kisabya Almas (Rais). na Mgombea Mwenza,  Hamisi Ally Hassan pamoja na Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP),Kunje Ngombale Mwiru (urais). Mgombea huyo wa AAFP aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe.  Shum Juma Abdalla.


 Tume inataraji kufanya uteuz

i wa wagombea Agosti 27 mwaka huu na kampeni zitaanza Agosti 28 hadi Oktoba 28, 2025. Uchaguzi Mkuu wa  Rais, wabunge na madiwani utafanyika Oktoba 29.







Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE....

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA