Leo na kesho zimebeba Maisha mapya ya Soka la ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) katika Soka la Afrika ambapo Mataifa Wenyeji wa Michuano Mataifa Bingwa Afrika (CHAN) Tanzania, Kenya na Uganda kuamua hatma yao.
Majira ya saa 11 jioni Kenya watashuka dimbani kumenyana na Madagascar mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya makala ya nane, huku majira ya saa 2:00 usiku Tanzania itakwatuana na Morocco katika Dimba la Benjamin Mkapa.
Robo Fainali ya tatu ni kesho pale Uganda wakipepetena na Senegal huku Visiwani Zanzibar Sudan wakionyeshana makali dhidi ya Algeria.
Hakika ni masaa 48 ya Afrika Mashariki na Kati Mabegani mwa Tanzania, Kenya, Uganda na Sudan kuandika rekodi mpya ya mashindano ya Afrika.
Comments