Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo akitumia usafiri wa Bajaji kuingia Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) eneo la Njedengwa Dodoma Agosti 10, 2025, kuchukua fomu za kuomba uteuzi huo.
Amesema kuwa vipaumbele vyake endapo akishinda urais vitakuwa; Afya, Ajira na Miundombinu.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo. Mgombea huyo wa NLD aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Chausiku Khatib Mohamed (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 10,2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima.
Wafuasi wa NLD wakiimba na kushangilia walipokuwa wakiingia kwenye viwanja vya INEC.
Doyo akipunga mikono alipowasili INEC.
Doyo akiwa na Mgombea Mwenza wa chama hicho, Chausiku Khatib Mohamed wakionesha mfuko wenye fomu hizo. .
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments