ADA - TADEA WACHUKUA FOMU ZA URAIS, WAJA NA FIRA YA TEKNOLOJIA

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Tanzania Democratic Alliance ( ADA-TADEA), Georges Gabriel Bussungu ambaye aliambatana na Mgombea Mwenza,  Ali Makame Issa.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu, Mgombea pendekezwa wa Urais wa chama hicho, Bussungu ametaja baadhi ya vipaumbele vya chama hicho kuwa ni,   atahakikisha analeta mabadiliko katika magaeuzi makubwa ya kiuchumi na Fikra ya Kiteknolojia.

Vyama vingine vilivyochukua fomu leo ni; Union for Multparty Democracy (UMD) ambacho wagombea wake wote ni wanawake, Mwajabu Noty Mirambo (Rais) na Mashavu Alawi Haji pamoja na Chama cha Tanzania Labour Party (TLP).

Wagombea wengine waliochukua fomu jan Agosti 10 ni;  Chama cha MAKINI ambacho wagombea wake ni Coster Jimmy Kibonde. na Mgombea Mwenza, Aziza Haji Suleiman,  National League for Democracy (NLD),  Doyo Hassan Doyo na Mgombea Mwenza,  Chausiku Khatib Mohamed na United Peoples Democratic Party (UPDP),  Twalib Ibrahim Kadege (Urais),  Mgombea Mwenza, Abdalla Mohd Khamisi.

Vyama vilivyofungua pazia ya uchukuaji fomu Agosti 9, 2025 ni; Chama Cha Mapinduzi (CCM) mgombea wake wa Urais ni Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza, Dkt. John Nchimbi, Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) walikuwa ni Hassan Kisabya Almas (Rais). na Mgombea Mwenza,  Hamisi Ally Hassan pamoja na Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP), Kunje Ngombale Mwiru (urais). Mgombea huyo wa AAFP aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe.  Shum Juma Abdalla.


 Tume inataraji kufanya uteuzi wa wagombea Agosti 27 mwaka huu na kampeni zitaanza Agosti 28 hadi Oktoba 28, 2025. Uchaguzi Mkuu wa  Rais, wabunge na madiwani utafanyika Oktoba 29.



Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Tanzania Democratic Alliance ( ADA-TADEA), Georges Gabriel Bussungu, akiwa na Mgombea Mwenza  Mgombea Mwenza, Mhe.  Ali Makame Issa (kushoto) wakionesha mkoba huo.

Bussungu akitia saini kuthibitisha kupokea fomu hizo.

 Mgombea Mwenza, Mhe.  Ali Makame Issa naye akitia saini.

Wagombea wakishangilia pamoja na wafuasi wao nje ya viwanja vya Tume.
Busungu akiingia kwenye gari tayari kuondoka eneo hilo.
Masafara wao ukiondoka INEC.
Shangwe zikiendelea kwenye viwanja vya Tume.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE....