NMB YATOA ELIMU KWA WAFANYABIASHARA WA DODOMA KUPITIA NMB BUSINESS CLUB

 Benki ya NMB imeendelea kuimarisha uhusiano wake na wateja wa kibiashara kwa kutoa elimu na ufafanuzi kuhusu huduma na masuluhisho mbalimbali ya kifedha kupitia NMB Business Club iliyoandaliwa jijini Dodoma jana.


Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara Makao Makuu ya NMB, Reynold Tony, alisema benki hiyo ina dhamira ya kuhakikisha wafanyabiashara wanapata uelewa mpana juu ya bidhaa na mipango ya kifedha inayotolewa na NMB ili kuongeza tija na ukuaji wa biashara zao.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Amos Mubusi, alisema mikutano ya aina hiyo ni fursa ya kipekee kwa benki na wafanyabiashara kubadilishana mawazo, changamoto na suluhisho, jambo linaloimarisha uhusiano wa kibiashara na kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa.

Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki walieleza kufurahishwa na mafunzo hayo, wakibainisha kuwa yamewasaidia kupata uelewa zaidi wa huduma za kifedha zenye manufaa kwa biashara zao, ikiwemo huduma za mikopo, bima, ulipaji kodi na suluhisho za kidijitali zinazorahisisha shughuli za kila siku.

Kupitia NMB Business Club, Benki ya NMB imekuwa ikiwafikia wafanyabiashara kote nchini kwa lengo la kuongeza maarifa ya kifedha na kuimarisha nafasi yao katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania.












Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE....

RC KIHONGOSI AELEZA MAFANIKIO LUKUKI MKOA ARUSHA

RAIS SAMIA AMUONDOLEA POLEPOLE HADHI YA UBALOZI

RAIS WA BURKINA FASO ATANGAZA DIRA YA KUUNDA MUUNGANO WA MATAIFA YA AFRIKA (UNITED STATES OF AFRICA).