Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akionesha kikapu chenye ujumbe huo muhimu wakati wa mkutano wa Kampeni za Mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Tambukaleli jijini Dodoma Agosti 31, 2025.
Akielezea baadhi ya mafanikio yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita na kuleta fursa za ajira katika mkoa huo ametaja kuwa ni; kuvutia wawekezaji kwa kujenga viwanda, Soko la Machinga, Barabara ya mzunguko, Reli ya SGR, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato na Uwanja wa mkubwa wa kisasa wa Mpira.
Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaahidi wakazi wa Dodoma kuwa endapo chama hicho kitapata ridhaa ya kuchaguliwa tena, kitaenda kumaliza tatizo la maji katika mkoa huo na kuwa hakutakuwa na shida ya maji.
Amesema changamoto hiyo ya maji itatatuliwa kupitia mradi mkubwa utakaoanza kutoa maji kutoka Ziwa Victoria mkoani Mwanza hadi Dodoma pamoja kukamilisha ujenzi wa bwawa kubwa la maji la Farkwa.
Kabla ya mkutano huo, Dkt. Samia leo amefanya mikutano ya kampeni Chamwino, Chemba na Kondoa.
Comments