KIKOSI cha Simba kimetembelea eneo la kihistoria la Piramidi ya Giza (Pyramids of Giza) ambalo lilitumiwa na watawala wa kale wa Misri, lakini pia kutembelea mto Nile.
Nile ni Mto mkubwa upande wa Mashariki ya bara la Afrika lna unatajwa kama Mto mrefu kabisa duniani kushinda Mto Amazonas.
Chanzo cha Mto Nile ni Mlima mkubwa wa Burundi, Luvironza lakini na maji ya Ziwa Victoria humiminika kwenye Mto huo unaopita miji ya Alexandria, Assuan, Atbara, Bahri, Fajum, Giza, Jinja, Juba, Cairo, Kampala, Khartum, Kigali, Kusti, Luxor, Malakal, Omdurman, Port Said, Rabak na Tanta.
Kutoka Ziwa la Victoria Nyanza hadi mdomo wake kwenye Bahari ya Mediteranea — Nile inavuka nchi za Uganda, Sudan Kusini, Sudan na Misri kwa urefu wa Kilomita 6,650.
Comments