TUMEVAA VIATU VYA MTIKILA, TUTAWAFUTA MACHOZI WALALAHOI - DP


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP), Abdul Juma Mluya na aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Masoud Aadoun Abrahman Khatib (kushoto) katika tukio lililofanyika  Agosti 13, 2025 Njedengwa jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima.


Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu, Mgombea pendekezwa wa Urais wa chama hicho,Mluya amesema kuwa wamevaa viatu vya aliyekuwa mwasisi wa chama hicho marehemu Christopher Mtikila kuwapambania walalahoi ili wapate nafuu ya maisha lakini pia watahakikisha wanawaongezea posho na mishahara Polisi na kuwapa likizo ya  miezi mitatu wajawazito wanapojifungua. Atawaboreshea mazingira ya kazi askari magereza.


Vyama vingine vinavyotarajiwa kuchukua leo fomu za Urais na umakamu wa Rais ni; Chama Cha Sauti ya Umma (SAU) na  The Civic United Front (CUF) Chama Cha Wananchi.

Vyama vingine vilivyochukua fomu leo ni; Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD) ambacho mgombea wake Urais ni Mwajuma Noty Mirambo aliyeambatana na Mgombea Mwenza,  Mashavu Alawi Haji pamoja na Chama cha Tanzania Democratic Alliance ( ADA-TADEA), ambacho mgombea urais ni Georges Gabriel Bussungu ambaye aliambatana na Mgombea Mwenza,  Ali Makame Issa.

Wagombea wengine waliochukua fomu juzi Agosti 10 ni;  Chama cha MAKINI ambacho wagombea wake ni Coster Jimmy Kibonde. na Mgombea Mwenza, Aziza Haji Suleiman,  National League for Democracy (NLD),  Doyo Hassan Doyo na Mgombea Mwenza,  Chausiku Khatib Mohamed na United Peoples Democratic Party (UPDP),  Twalib Ibrahim Kadege (Urais),  Mgombea Mwenza, Abdalla Mohd Khamisi.

Vyama vilivyofungua pazia ya uchukuaji fomu Agosti 9, 2025 ni; Chama Cha Mapinduzi (CCM) mgombea wake wa Urais ni Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza, Dkt. John Nchimbi, Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) walikuwa ni Hassan Kisabya Almas (Rais). na Mgombea Mwenza,  Hamisi Ally Hassan pamoja na Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP),Kunje Ngombale Mwiru (urais). Mgombea huyo wa AAFP aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe.  Shum Juma Abdalla.


Tume inataraji kufanya uteuzi wa wagombea Agosti 27 mwaka huu na kampeni zitaanza Agosti 28 hadi Oktoba 28, 2025. Uchaguzi Mkuu wa  Rais, wabunge na madiwani utafanyika Oktoba 29.


Kailima akiwaelekeza wagombea jinsi ya kujaza kwenye kitabu cha rejesta.


Mluya akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu.

Msafara ukiondoka  baada ya mchakato wa kuchukua fomu.





 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE....

RAIS SAMIA AMUONDOLEA POLEPOLE HADHI YA UBALOZI