UDP WACHUKUA FOMU ZA URAIS INEC, KUENDELEZA SERA YA KUWAMWAGIA PESA WANANCHI

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha  United Democratic Party (UDP), Saum Hussein Rashid  aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Juma Khamis Faki  katika tukio lililofanyika  Agosti 15, 2025 Njedengwa jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhan Kailima.


Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu, Mgombea pendekezwa wa Urais wa chama hicho, Saum amesema kuwa chama chake kikishinda kitaendaleza sera yake ya kuwamwagia fedha wananchi, kitadumisha amani na utulivu wa Nchi.

Aidha, amesema kuwa kwa vile yeye ni mwanamke atahakikisha wanaenda kutatua changamoto zote zinazowabagua wanawake katika sera na sheria ili kutokomeza ukatili wa kijinsia kwama kwamba rasilimali ziweze kuwanufaisha wananchi wote wanawake na wanaume. 

 Vyama vingine vilivyochukua fumu Agosti 13, 2025 ni; Chama cha Democratic Party (DP), Abdul Juma Mluya (Urais) aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Masoud Abrahman Khatib na  Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Paul Kyara (Urais) aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Satia Mussa  Bebwa.

Vilivyochukua fomu Agosti 12, 2025 ni; Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD) ambacho mgombea wake urais ni Mwajuma Noty Mirambo aliyeambatana na Mgombea Mwenza,  Mashavu Alawi Haji pamoja na Chama cha Tanzania Democratic Alliance ( ADA-TADEA), ambacho mgombea urais ni Georges Gabriel Bussungu aliyeambatana na Mgombea Mwenza,  Ali Makame Issa.

Wagombea wengine waliochukua fomu  Agosti 10, 2025 ni;  Chama cha MAKINI ambacho wagombea wake ni Coaster Jimmy Kibonde. na Mgombea Mwenza, Aziza Haji Suleiman,  National League for Democracy (NLD),  Doyo Hassan Doyo (Urais) na Mgombea Mwenza,  Chausiku Khatib Mohamed pamoja na United Peoples Democratic Party (UPDP),  Twalib Ibrahim Kadege (Urais),  Mgombea Mwenza, Abdalla Mohd Khamisi.

Vyama vilivyofungua pazia ya uchukuaji fomu Agosti 9, 2025 ni; Chama Cha Mapinduzi (CCM) mgombea wake wa Urais ni Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza, Dkt. John Nchimbi, Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) walikuwa ni Hassan Kisabya Almas (Rais). na Mgombea Mwenza,  Hamisi Ally Hassan pamoja na Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP),Kunje Ngombale Mwiru (urais). Mgombea huyo wa AAFP aliambatana na Mgombea Mwenza,  Shum Juma Abdalla.Hadi leo hii vyama vilivyochukua fomu ni 12.


Tume inataraji kufanya uteuzi wa wagombea Agosti 27 mwaka huu na kampeni zitaanza Agosti 28 hadi Oktoba 28, 2025. Uchaguzi Mkuu wa  Rais, wabunge na madiwani utafanyika Oktoba 29.


Kailima akimuelekeza Saumu jinsi ya kujaza kwenye rejesta kuthibitisha kwamba wamechukua fomu hizo.

Wafuasi wa chama UDP wakishangilia walipowasili Tume kuchukua fomu.

 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE....

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

RAIS SAMIA AMUONDOLEA POLEPOLE HADHI YA UBALOZI