WAGOMBEA UPDP WACHUKUA FOMU ZA URAIS INEC, KIPAUMBELE CHAO NI ARDHI


Wateule wa Chama Cha UPDP wakitoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Njedengwa Dodoma, Agosti 10, 2025 baada ya kuchukua fomu za kuomba uteuzi wa kugombea urais na umakamu wa Rais Tanzania.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha United People's Democratic Party (UPDP), Mhe. Twalib Ibrahim Kadege. Kadege  aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe.  Abdalla Mohamed Khamisi (kushoto) wakati wa kuchukua fomu hizo leo Agosti 10, 2025.

Wagombea wengine waliochukua fomu leo ni kutoka vyama vya; MAKINI ambacho wagombea wake ni Coster Jimmy Kibonde. na Mgombea Mwenza, Aziza Haji Suleiman,  National League for Democracy (NLD),  Doyo Hassan Doyo na Mgombea Mwenza,  Chausiku Khatib Mohamed na United Peoples Democratic Party (UPDP),  Twalib Ibrahim Kadege (Urais),  Mgombea Mwenza, Abdalla Mohd Khamisi.

Vyama vilivyofungua pazia ya uchukuaji fomu Agosti 9, 2025 ni; Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho mgombea wake wa Urais ni Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza, Dkt. John Nchimbi, Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) walikuwa ni Hassan Kisabya Almas (Rais). na Mgombea Mwenza,  Hamisi Ally Hassan pamoja na Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP), Kunje Ngombale Mwiru (urais). Mgombea huyo wa AAFP aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe.  Shum Juma Abdalla.

 
Jumatatu Agosti 11, 2025 itakuwa zamu ya vyama vya;African Democratic Alliance Party (ADA TADEA), Union forMultparty Democracy (UMD) na Tanzania Labour Party (TLP).

 Tume inataraji kufanya uteuzi wa wagombea Agosti 27 mwaka huu na kampeni zitaanza Agosti 28 hadi Oktoba 28, 2025. Uchaguzi Mkuu wa  Rais, wabunge na madiwani utafanyika Oktoba 29.
Baadhi ya wafuasi wao.

Mgombea urais Kadege akizungumz na waandishi wa habari na kutaja vipaumbele vyao kuwa ni Ardhi na Afya.

Wakiondoka baada ya kuchukua fomu.




 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE....