
Wagombea wapendekezwa wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Salumu Mwalimu (Rais) na Devotha Minja (Makamu wa Rais) wakishangiliwa na wafuasi wao walipokuwa wakiingia Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Njedengwa Dodoma Agosti 12, 2025, kuchukua fomu za kuomba uteuzi huo.
Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu, Mgombea pendekezwa wa Urais wa chama hicho,Mwalimu ambaye alisindikizwa na umati wa watu amesema kuwa Ilani yao imebebwa na kipaumbele chao kikubwa ambacho nikujenga uchumi imara wa kuwapunguzia wananchi umasikini wa kipato.
Vyama vingine vilivyochukua fomu leo ni; Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD) ambacho mgombea wake Urais ni Mwajuma Noty Mirambo aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Mashavu Alawi Haji pamoja na Chama cha Tanzania Democratic Alliance ( ADA-TADEA), ambacho mgombea urais ni Georges Gabriel Bussungu ambaye aliambatana na Mgombea Mwenza, Ali Makame Issa.
Wagombea wengine waliochukua fomu juzi Agosti 10 ni; Chama cha MAKINI ambacho wagombea wake ni Coster Jimmy Kibonde. na Mgombea Mwenza, Aziza Haji Suleiman, National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo na Mgombea Mwenza, Chausiku Khatib Mohamed na United Peoples Democratic Party (UPDP), Twalib Ibrahim Kadege (Urais), Mgombea Mwenza, Abdalla Mohd Khamisi.
Vyama vilivyofungua pazia ya uchukuaji fomu Agosti 9, 2025 ni; Chama Cha Mapinduzi (CCM) mgombea wake wa Urais ni Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza, Dkt. John Nchimbi, Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) walikuwa ni Hassan Kisabya Almas (Rais). na Mgombea Mwenza, Hamisi Ally Hassan pamoja na Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP),Kunje Ngombale Mwiru (urais). Mgombea huyo wa AAFP aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Shum Juma Abdalla.
Tume inataraji kufanya uteuzi wa wagombea Agosti 27 mwaka huu na kampeni zitaanza Agosti 28 hadi Oktoba 28, 2025. Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utafanyika Oktoba 29.

Baadhi ya wajumbe na watendaji wa Tume wakishuhudia tukio hilo.
Mwalimu akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu.
Wakiondoka baada ya kuchukua fomu, huku mgombea urais Mwalumu akiungana na wafuasi kupiga ngoma.
Comments