WASIFU WA SPIKA MSTAAFU HAYATI JOB NDUGAI

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai amefariki dunia leo Agosti 06, 2025 hospitalini wakati akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimetangazwa na Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson.

Job Yustino Ndugai alikuwa mwanasiasa kutoka Tanzania ambaye alihudumu kama Spika wa Bunge tangu mwaka 2015. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.

Alizaliwa Januari 21, 1963 alipata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.

Alisoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).

Alisoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).

Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008).

Hayati Ndugai alikuwa mbunge wa Kongwa kwa miaka 25 (tangu mwaka 2000) na alishika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.

Alichaguliwa kuwa spika wa bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika.

Moja ya mambo yatakayo kumbukwa akiwa katika uongozi wake wa bunge, ni pamoja na mijadala kadhaa ikiwemo sakata la wabunge 19 wa CHADEMA waliokuwa wamevuliwa uanachama wao, na kuhojiwa kwa baadhi ya wabunge akiwemo Josephat Gwajima na Jerry Muro kwa madai ya kushusha hadhi na heshima ya bunge.

Mbali na ubunge, Hayati Ndugai alifanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Januari 6, 2022 alijiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.

Hayati Job Ndugai alikuwa akiwania kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo Kongwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE....