Wataalamu 69 wa reli kutoka Tanzania wanatarajiwa kushiriki mafunzo ya siku 80 katika Chuo Kikuu cha Jiaotong, Beijing – China, yenye lengo la kuongeza ujuzi wao juu ya Reli ya Kisasa ya Standard Gauge (SGR).
Uhusiano kati ya China na Tanzania una historia ndefu ya ushirikiano wa miundombinu na maendeleo. Kuanzia mradi wa reli ya TAZARA miaka ya 1970 hadi uwekezaji wa sasa kwenye SGR, China imekuwa mshirika muhimu katika kusaidia Tanzania kukuza sekta ya usafirishaji na biashara.
Hatua ya kuwapeleka wataalamu wa Kitanzania China kwa mafunzo inaonyesha kuwa ushirikiano huu si wa kiufundi tu, bali pia ni wa kujenga uwezo wa ndani (capacity building).
Hii ni ishara kwamba:
• Tanzania inalenga kuwa na wataalamu wake wazawa wenye ujuzi wa uendeshaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama Reli ya kisasa (SGR) na uendeshaji wa Treni za umeme badala ya kutegemea wageni muda wote.
• China inaendeleza Diplomasia yake na Tanzania kwa kuwekeza kwenye Elimu na ujuzi kwa watanzania.
• Ushirikiano huu unaimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kimkakati kati ya Nchi hizi mbili.
• TRC wamechangamkia fursa ni hatua nzuri zaidi kuboresha utendaji wake.
Embassy of China in Tanzania
Comments