Mheshimiwa Majaliwa asema Simbu ameliheshimisha Taifa
▪️Atoa zawadi kwa Timu zilizofanya vizuri kimataifa
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza Mwanariadha Alphonse Simbu kwa kuwa Bingwa wa Dunia wa mbio za marathon za Tokyo na kwamba ataendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya michezo ili itoe mchango zaidi katika kukuza uchumi wa nchi na kuongeza wigo wa upatikanaji ajira kwa vijana
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumamosi (Septemba 27, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla kuwapongeza wanamichezo na timu zilizofanya vizuri kwenye medani za kimataifa, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa hotel jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo Mheshimiwa Majaliwa alitangaza kuwa, Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia amempatia Mwanariadha Simbu zawadi ya nyumba jijini Dodoma, sambamba na kikabidhiwa kitita cha shilingi milioni 20 ikiwa ni ishara ya kutambua ushindi huo ambao umeliletea Taifa heshima kwenye jukwaa la kimataifa”
“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameandaa nyumba iliyopo mkoani Dodoma, ambayo itakabidhiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na zoezi hilo lisichukue muda mrefu kuanzia leo, tusiwe tunatamka ahadi za viongozi halafu zinakaa muda ambao mtu anajiuliza”
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Mwanariadha Simbu ameandika ukurasa wa upekee kwa kuwa mtanzania wa Kwanza kutwaa tuzo ya dhahabu katika marathoni ya Dunia ya mwaka 2025 “Haya ni Mashindano makubwa zaidi ya riadha duniani baada ya Michezo ya Olympic, yakihusisha wanariadha Bora kutoka Mataifa yote duniani”
Comments