🟩🟨⬛️
KOCHA MKUU wa klabu ya wiliete Benguela iliyoondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na Young Africans, amefunguka mengi baada ya mchezo wa jana kumalizika. Kocha huyo amesema ubora wa kikosi chake huwezi kufananisha kabisa na kikosi cha Yanga kilichosheheni wachezaji wenye uwezo mkubwa. Anasema wachezaji wa Yanga ni wa daraja la juu (wanaoanza hata wale waliopo benchi), hivyo kwao ulikuwa ni mtihani mgumu kukabiliana na miamba hii ya soka la Tanzania.
🔰...Aidha, Kocha Bruno Ferry amemtaja Pacome Zouzoua kama mmoja wa wachezaji hatari sana waliopo kwenye kikosi cha Yanga SC. Amesema Pacome ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kufanya lolote wakati wowote awapo uwanjani. Mwisho kabisa Kocha huyo aliyewahi kuinoa klabu ya Azam FC ameweka wazi kuwa anaiona Yanga ikifika mbali kwenye michuano hii ya Klabu Bingwa Afrika.
Comments