Na Richard Mwaikenda, Songea
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kujenga Chuo Cha Uhasibu Kampasi ya Arusha mkoani Ruvuma
Rais Dkt. Samia ametoa ahadi hiyo alipokuwa akijinadi katika mkutano wa Kampeni za CCM kwenye viwanja vya Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Songea Mjini leo Septemba 22, 2025.
Amesema kuwa ujenzi wa Chuo hicho ukikamilika Chuo kitakuwa na uwezo kuchukua kwa mkipuo zaidi ya wanafunzi 10,000, hivyo wana Ruvuma wajiandae kuwa wahasibu.
Comments