Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk Emmanuel Nchimbi amewasili Songea, mkoani Ruvuma leo Septemba 19, 2025.
Dk Nchimbi ataungana tena na Mgombea urais wa chama hicho, Dkt.Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuwasili kesho ambapo watakutana mkoa mmoja tangu Agosti 28, mwaka huu walipozindua kampeni za chama hicho kitaifa mkoani Dar es Salaam.
Baada ya uzinduzi,Dkt. Samia na Dk Nchimbi waligawana maeneo kwenda kunadi Ilani ya CCM na kueleza kile walichokifanya miaka mitano iliyopita na wanachotarajia kukifanya endapo watachaguliwa.
Baada ya uzinduzi, Samia yeye alianzia Morogoro, Dodoma, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Singida, Tabora, Kigoma na mikoa mitatu kati ya mitano ya Zanzibar ambayo ni, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja na Kusini Pemba.
Dk Nchimbi yeye alianza kwa watani zake kanda ya ziwa mikoa wa Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita, Kagera, Rukwa, Katavi, Arusha, Kilimanjaro, Tanga na sasa anaingia nyumbani mkoani Ruvuma.
Comments