𝗥𝗔𝗜𝗦 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗔𝗠𝗘𝗪𝗔𝗝𝗘𝗡𝗚𝗘𝗔 𝗪𝗔𝗡𝗔𝗪𝗔𝗞𝗘 𝗠𝗢𝗬𝗢 𝗪𝗔 𝗨𝗝𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜 𝗡𝗔 𝗞𝗨𝗝𝗜𝗔𝗠𝗜𝗡𝗜


𝘼𝙢𝙚𝙚𝙡𝙚𝙯𝙖 𝙆𝙖𝙩𝙞𝙗𝙪 𝙈𝙠𝙪𝙪 𝙢𝙨𝙩𝙖𝙖𝙛𝙪 𝙬𝙖 𝘾𝘾𝙈, 𝘿𝙠𝙩. 𝘽𝙖𝙨𝙝𝙞𝙧𝙪 𝘼𝙡𝙡𝙮


"Kwa muda mrefu katika historia ya siasa Duniani kote, nafasi ya mwanamke imekuwa nafasi ya pili kanakwamba utu wake ni nusu..duniani kote ajenda ya kuweka usawa kwa wanaume na wanawake imekuwa mfupa mgumu.."


"..CCM kwasababu ya msimamo wetu wa kifalsafa na kiitikadi, usawa wa wanaume na wanawake si suala la hiari ni saula la lazima.."


"..katika uongozi wako Rais Dkt. Samia...kitakwimu katika kipindi ulichoingia kama Mkuu wa nchi na Mwenyekiti wa chama (CCM) , kitakwimu angalieni maamuzi, sera, miradi na namna utekelezaji wake ulivyoinua hali za akina Mama.."


Dkt. Bashiru ameyasema hayo leo tarehe 9 Septemba 2025 wakati akizungumza na maelfu ya Wananchi wa Singida Mjini waliojitokeza katika uwanja wa Bombadia kumlaki na kumsikiliza Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻.


Aidha, Dkt. Bashiru ameeleza kuwa hivi sasa Tanzania nafasi ya mwanamke imekuwa sawia na mwanaume na si kwamba Rais Dkt. Samia amekuwa akiwapendelea la hasha bali amewajengea uwezo mkubwa wanawake wa ujasiri, kufanya kazi na kujiamini.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI

CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-

RC KIHONGOSI AELEZA MAFANIKIO LUKUKI MKOA ARUSHA

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA