*1. Usiweke Akiba Mwishoni Weka Mwanzoni*
Watu wengi wanasubiri walipwe mishahara au kupata faida ndipo waanze “kuona kama kimebaki” ili waweke akiba. Hii ni kosa..
Weka akiba mara tu unapopokea kipato (10%–20% ya mapato yako).
*2.Usitumie Pesa Yote Jifunze Kuishi Chini ya Kipato*
Ukiwa na kipato cha 1M, usipange matumizi ya 1M. Panga matumizi ya 700k–800k.
Unapojilazimisha kuishi chini ya kipato chako, unajilinda dhidi ya dharura na kuacha nafasi ya kuwekeza.
*3.Kuwa na Vyanzo Zaidi ya Kimoja cha Mapato*
Hata ukiwa na kazi nzuri, biashara ndogo au uwekezaji mdogo ni ngao ya kifedha.
Mfano: Mwalimu mwenye mshahara anaweza kuwa na shamba la nyanya au kuuza mtandaoni.
*4.Epuka Madeni Mabaya*
Kuna madeni mazuri (yanayokuongezea kipato, kama mkopo wa mashine ya biashara) na mabaya (kukopa kwenda kwenye sherehe au kununua simu ya anasa)
Deni baya ndilo chanzo kikuu cha watu kuishiwa pesa kila wakati
*5.Wekeza Badala ya Kuweka tu Akiba*
Akiba inalinda lakini haitaikuza pesa yako.
• Uwekeze sehemu kama:
• Hisa (mfano DSE – CRDB, NMB)
• Mifuko ya pamoja (UTT AMIS M-Wekeza)
• Ardhi na nyumba (real estate)
• Biashara ndogo zinazojirudia.
*6.Jifunze Kudhibiti “Impulse Buying” (Matumizi ya Hasira na Raha)*
Usinunue vitu kwa sababu tu umeviona, ongeza tabia ya “nitakuwazia kesho” kabla ya kununua kitu kisicho cha lazima.
Hii inalinda pesa yako isivuje kama maji kwenye ndoo yenye tundu.
*7.Jenga Mifumo ya Kifedha (Budget + Record Keeping)*
Ukiwa na daftari au app ya kufuatilia pesa zako, utaona zinapotea wapi.
Wengi wanaishiwa sio kwa sababu hawapati pesa, bali kwa sababu hawajui zinapotelea wapi.
Mwisho . Kuwa na Nidhamu ya Muda Mrefu
*Zingatia hili Hata ukiwa na mbinu zote, bila nidhamu utarudi palepale.*
Matajiri na watu waliokomaa kifedha wanashinda kwa nidhamu ya muda mrefu, siyo kipato kikubwa tu.
👉 Kwa kifupi: usiishiwe pesa = jifunze kudhibiti matumizi + uwe na vyanzo vingi + akiba + uwekezaji + nidhamu
*#MaarifaYaUwekezaji📚*
_Jacob Mahundi ✍️_
Comments