"Miaka 12 iliyopita nilipata fursa ya kujifunza diplomasia na ustahimilivu kupitia aliyekuwa Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa [SUKI] Dr. AshaRose Migiro. Alinitaka muda wote kutenda kwa kuandaa maandiko na kuyasaili kisha ndipo nitende. Shule ile ilinikaa na kunifanya muda wote nikikutana naye hata baada ya kuhama ofisi moja na nyingine nimkumbuke kama mwalimu imara. Miaka imeenda na siku zikasonga mbele."
"Leo ameaminiwa kushika nafasi ya juu ya utendaji ya CCM. Nafasi ambayo nami nilishaitumikia kabla ya mtangulizi wake. Hakika nimefurahi kuona Mwalimu akikabidhiwa darasa kufundisha. Kazi muhimu ni wanafunzi kubeba utayari. Karibu tena nyumban SG mpya."
"Sisi tupo tayari kutumwa. Picha hii ni kumbukumbu ya mimi na SG mpya katika mkutano Mkuu uliopita." #KaziNaUtuTunasongaMbele #NaendeleaKujifunza
Comments