Baada ya uzinduzi wa kampeni kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam Agosti 28, 2025 leo mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaingia kwa kishindo mkoa wa tisa wa Kigoma baada ya kufanikisha kwa kiwango cha hali ya juu kampeni katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Singida na leo mchana Tabora.


Anaingia mkoa huo maarufu kwa kilimo cha michikichi kwa ajili ya mafuta, uvuvi ziwa Tanganyika.

Anaingia Mkoa huo kifua mbele kutokana na Serikali anayoiongoza ikiwa umetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

 Kigoma ni Kati ya Mikoa michache sana ambayo Ina miradi Mingi sana ya Maendeleo.Ndani ya miaka 4 ya Rais Samia Mkoa huo umepokea zaidi ya Trilioni 11 kwenye sekta mbalimbali za maendelea

‎Baadhi ya miradi mikubwa ya Maendeleo inayoendelea na utekelezwaji Mkoani Kigoma ni hii ifuatayo,

‎Ujenzi wa Barabara Kuu za lami zaidi ya km 420 zikiwemo za Kibondo-Mabamba na Kibondo-Marongwe

‎Ujenzi wa Barabara za mitaa km 10 chini ya Tactic

‎Ujenzi na Ukarabati wa Bandari ya Lagosa,Kibirizi

‎Ujenzi wa meli Mpya na Chelezo ya Kuundia meli

‎Ukarabati wa meli za mv Sangara na Mv Liemba Ziwa Tanganyika

‎Ujenzi wa Station kuu ya Sgr Kigoma

‎Ujenzi wa SGR Tabora-Kigoma(Main Camp ni Uvinza-Kigoma)

‎Ujenzi wa Soko Kuu la Mwanga na soko la Katonga via Tactic

‎Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu Cha Muhimbili

‎Ujenzi wa Tawi la Chuo Cha Uhasibu TIA

‎Upanuzi wa Chuo Cha Taifa Cha Hali ya hewa na Ufungaji wa radar

‎Ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi

‎Ujenzi,ukarabati na upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Kigoma (Gombe-Mahare International Airport)

‎Ujenzi wa njia kubwa ya kusafirisha Umeme wa Kv 400 Nyakanazi-Kidahwe

‎Ujenzi wa Tawi la BoT Kanda ya Magharibi(Usanifu unaendelea)

‎Construction of Katosha Dry Port

‎Ujenzi wa meli Mpya ya abiria na Mizigo

‎Ujenzi wa meli ya Abiria

‎Ujenzi wa Chuo Cha Umahili wa Tehama Buhigwe

‎Miradi kedekede ya Maji ya zaidi ya Bilioni 429

‎Ujenzi wa Malagarasi Hydropower Project

‎*Ujenzi wa kiwanda Kipya Cha Saruji Cha Tanzania Cement Company ltd

‎*Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda Cha Pamba na Kiwanda Cha Sukari Kasulu Sugar

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI

CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-

RC KIHONGOSI AELEZA MAFANIKIO LUKUKI MKOA ARUSHA

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA