Alikuwa masikini akiwa na miaka 52. Akawa Bilionea akiwa na miaka 59. Hivi ndivyo Ray Kroc alivyofanya.
Muuzaji aliyefeli akiwa na miaka 52 alifanikiwa kujenga mtandao mkubwa zaidi wa migahawa duniani.
Ray Kroc alikuwa akiendesha Cadillac yake akizunguka Amerika akiuza mashine za kutengeneza milkshake.
Kwa miaka 17.
Alikuwa na miaka 52. Ameachika. Hana pesa. Anaumwa mishipa(arthritis). Kisukari.
Na hakuna aliyekuwa akinunua mashine zake.
Watu wengi wa umri huo walikuwa wakifikiria kustaafu.
Kisha siku moja alipokea simu iliyobadilisha kila kitu.
Kibanda cha burger kule California kilihitaji mashine zake nane.
Nane. Hakuna mtu aliyewahi kuagiza mashine nyingi hivyo.
Alilazimika kwenda kukiona kwa macho.
Aliendesha hadi San Bernardino. Akafika kwenye jengo dogo lenye umbo la pembe nane na matao ya dhahabu.
Akaona kitu ambacho hakikuonekana kuwa cha kawaida.
Ndugu wawili walikuwa wakihudumia burger na viazi(chips) kwa sekunde 30. Kwa ukamilifu kila wakati. Ubora ule ule. Kasi ile ile.
Foleni haikuisha.
Kroc aliwauliza wale ndugu jinsi walivyofanikiwa.
Walimwonyesha mfumo wao. Upishi wa mtindo wa laini ya uzalishaji. Menyu ndogo. Ufanisi wa juu.
Wengine wote waliona ni kibanda cha kawaida cha burger kilichofanikiwa.
Kroc aliona mfumo unaoweza kuigwa. Kupanuliwa. Kurudiwa kila mahali.
Hiki ndicho Kroc alichokielewa ambacho ndugu hao wa McDonald hawakukiona:
Thamani haikuwa kwenye mgahawa mmoja. Thamani ilikuwa kwenye mfumo wenyewe.
Aliwashawishi waanzishe mfumo wa franchising. Walikuwa na hofu. Walikuwa wamewahi kujaribu hapo awali na walichukia kushughulika na wamiliki wa franchise.
Lakini Kroc hakukoma.
Mwaka 1955, akiwa na miaka 52, alifungua mgahawa wake wa kwanza wa McDonald’s huko Des Plaines, Illinois.
Hakufungua tu mgahawa. Alishikilia na kufuatisha kila kitu kama wale ndugu wa McDonald.
Alikuwa mwenyewe anatoa taka kwenye maegesho. Alipima muda wa kila hatua. Alihakikisha waraghbishi(franchisees) wake wanafuata mfumo kwa ukamilifu.
Ubora. Huduma. Usafi. Kasi.
Hakuna njia za mkato. Hakuna msamaha.
Kwa miaka mingi, hakupata pesa yoyote ya maana. Aliishi kwa kipato cha mkewe. Alikaribia kufilisika mara kadhaa.
Wale ndugu walipokea ada zao. Na Kroc alipata senti chache.
Lakini aliendelea kufungua migahawa. Akaendelea kuuboresha mfumo. Akaendelea kusonga mbele.
Kisha akagundua kiini halisi cha biashara.
Ardhi.
Nunua ardhi. Wape waraghbishi(franchisees) kwa kukodisha. Dhibiti kila kitu.
Hapo ndipo McDonald’s ilipoanza kulipuka.
Mwaka 1961, akiwa na miaka 59, Kroc alinunua biashara yote ile ya ndugu wa McDonald kwa dola milioni 2.7.
Na hapo ndipo ilipokua kama kaanza tena.
Aliendelea kujenga. Aliendelea kupanua. Aliendelea kuboresha uendeshaji.
Akaanzisha Big Mac. Egg McMuffin. Drive-thru. Maeneo ya michezo kwa watoto.
Kila ubunifu ulikuwa kwa lengo la kuhudumia watu wengi zaidi kwa kasi.
Alipokufa mwaka 1984, McDonald’s ilikuwa na migahawa zaidi ya 7,500.
Leo, McDonald’s inahudumia karibu wateja milioni 70 kila siku.
Katika nchi zaidi ya 100.
Zaidi ya maeneo 38,000 duniani kote.
Yote haya yalitokea kwa sababu muuzaji aliyekuwa anahangaika akiwa na miaka 52 alikataa kukubali hali yake ya kutokuwa na mafanikio.
Aliona mfumo wakati wengine waliona kibanda cha burger.
Alifanya kazi wakati wengine wangeamua kustaafu.
Alijitoa wakati wengine wangeamua kuondoka.
Ni fursa gani unayopuuza kwa sababu unaangalia juu juu badala ya mfumo?
Ni biashara gani unaiweka pembeni kwa sababu unafikiri kuwa wewe ni mzee sana au umechelewa?
Kroc alikuwa na miaka 52, maskini, na mgonjwa alipokutana na McDonald’s.
Alifanya kazi kwa bidi ya ajabu. Akajenga polepole. Hakuwahi kukata tamaa.
Kwa sababu alielewa jambo ambalo watu wengi hawalielewi.
Umri si tatizo. Kukata tamaa ndilo tatizo.
Kuwa maskini si mwisho. Bali kubakia maskini ndio mwisho.
Acha kufikiri kuwa miaka yako bora imekwishapita.
Anza kufikiri kama Ray Kroc.
Tafuta mfumo wako. Kamilisha mchakato wako. Panua bila kusita.
Na usimruhusu mtu yeyote akuambie umechelewa kujenga himaya yako.
Mara nyingi utajiri mkubwa hujengwa na watu wanaokataa kustaafu.
Kwa sababu ukiwa na miaka 52 na huna kitu, una chaguo mbili:
Kukata tamaa au kujitoa kikamilifu.
Ray Kroc alijitoa kikamilifu.
Na akabadilisha dunia.
Fikiria Kikuu.

Comments