Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameungana na Rais wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traoré kwa kile walichokiita Ukombozi wa Afrika kutoka kwa ukoloni mamboleo.
Hii ilidhihirika baada ya Traoré kupokea ujumbe wa Wana-Pan-Africanists unaoongozwa na Rais wa zamani wa Afrika Kusini katika ikulu ya Ouagadougou.
Walijadili ushirikiano wa kiuchumi, usalama wa kikanda, na mapambano ya kudhoofisha ushawishi usiofaa wa kigeni katika nchi za Afrika.
Jacob Zuma, ambaye alitawala Afrika Kusini kuanzia 2009 hadi 2018 na sasa anaongoza chama cha Upinzani cha MK, alisifu mtindo wa Uongozi wa Traoré na maono wazi ya Afrika inayojitegemea na iliyoungana, na kutoa mshikamano wake na kujitolea kuendeleza ajenda ya Pan-Africanist.

Comments