Mbunge Mteule wa Ilala, Mussa Azzan Zungu amechaguliwa kwa kishindo kuwa Mgombea wa Spika la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi uliomalizika Dodoma leo Novemba 9, 2025.
Zungu ambaye alikuwa Naibu Spika amepata Kura 348 akimshinda mpinzani wake Stephen Masele aliyepata kura 16.
Mbunge Mteule wa Babati Vijijini, Daniel Sillo amechaguliwa kuwania Unaibu Spika kupitia Chama hicho kwa kupata kura 362. Aliokuwa akigombea nao walijitoa.
Uchaguzi wa Spika na Naibu Spika wa Bunge utakaoshirikisha wagombea wengine kutoka vya upinzani utafanyika katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Bunge wa 13 baada ya wabunge wateule kuapishwa.
Uchaguzi huo wa ndani ya CCM ambao wapiga kura walikuwa wabunge wote wateule wa Chama hicho, ulifunguliwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Balozi Asha-Rose Migiro na kusinamiwa na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, John Mongella.
Spika anayemaliza muda wake ambaye pia alijitoa kwenye kinyang'anyiro hicho, Dkt Tulia Ackson alishuhudia uchaguzi huo.

Comments